Saturday, 5 November 2016

Jiamini Jikubali Utafanikiwa.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na safari yako ya kuyatafuta mafanikio.
Nikushukuru pia kwa kutembelea blog hii ili kuongeza maarifa.

Mpendwa msomaji Leo nitaongelea makala inayohusu kujiamini na kujikubali.
Kujiamini na kujikubali ni mambo ambayo uenda sawa kabisa, na moja likikosa lingine haliwezi kukamilika.
Kujiamini ni nguvu ya ndani kabisa(inner power) ambayo umfanya mtu aweze kusema anaweza jambo Fulani. Ukijiamini lazima utakuwa unajikubali tu.

Mwanamuziki Benpol aliwahi kuimba wimbo unaoitwa jikubali, umo alikuwa akiwaasa watu wajikubali, wapambane wanaweza kuwa kama watu wengine waliofanikiwa.

Je mtu anayejikubali na kujiamini yupoje?.
Huyu ni mtu ambaye upambana kila siku ya maisha yake, hakati tamaa na anajua wazi kwamba kushuka na kupanda kupo katika maisha ya mwanadamu ya kila siku.

Mtu anayejiamini na kujikubali si mfungwa wa matumaini(prisoner of hope). Mfungwa wa matumaini ni yule mtu ambaye kila muda anaota na kutamani kipaji au kipawa cha mtu mwingine. Wafungwa wa matumaini ni wale ambao utumaini Siku moja watatembea barabarani au mitaani na kuokota boksi au begi lenye bahati zao ndani. Mwandishi wa kitabu cha "See you at the top" bwana Zig Ziglar anasema "kitu kimojawapo kinachosikitisha maishani  ni kusikia mtu akisema 'kama ningeongea,kimbia,ruka, imba, cheza, waza kama yeye halafu sauti ubadilika na kuingia katika ukimya mkubwa.

Jambo jingine la msingi ili kujikubali na kujiamini lazima ujitambue wewe ni nani. Ukijitambua unaweza kuleta mabadiliko muda mfupi.

Hii ndio njia sahii ya kujitambua kwa mtu anayetaka kufanikiwa;
Chukua penseli andika uongo kuhusu wewe. Mfano; Mimi sio tajiri, siwezi kuwa na marafiki wazuri, siwezi kufaulu mitihani, siwezi kuwa mchezaji/muimbaji bora, na kadhalika. Soma uongo huo siku mbili kisha geuza uwe ukweli. Hapa chukua peni nyekundu na andika kinyume cha uongo uliouandika. Futa uongo uliouandika na kila siku soma ukweli uliouandika. Ukifanya ilo zoezi muda mrefu nakuhakikishia utaona mabadiliko na utaweza kujitambua na utakua mtu wa kujitambua na kujikubali siku zote na maisha yako yatakuwa ya furaha siku zote.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.

Tuwasiliane: 0764145476.
Whatsapp; 0625951842
Instagram; @eddybide

Tukutane kesho tena kwa mada nzuri kama hii.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: