Thursday, 3 November 2016

Mafanikio Yako Mikononi Mwako.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kuwa Unaendelea vizuri na kupambana kuelekea mafanikio.

Karibu katika makala ya Leo inayosema "mafanikio yako mikononi mwako". Nianze na hadithi moja ambayo ipo hivi, katika kijiji kimoja alikiwepo mzee mmoja mwenye busara na akili nyingi sana (genius). Siku moja Kijana mmoja alimchukua ndege na kwenda nae kwa mzee huyo akiwa amemficha mikononi. Alipofika kwa mzee alimuuliza mzee "je huyu ndege kwenye mkono wangu yupo hai au amekufa?". Aliuliza ili kuona kweli kama mzee ana akili nyingi kama watu walivyomsema. Mzee alimjibu kijana hivi; "nikisema yupo hai unamminya afe na nikisema amekufa utamuachia aruke apae juu angani, uhai wa ndege huyo yupo mikononi mwako". Na Mimi nasema mafanikio yako mikononi mwako.

Niamini Mimi nisemayo kwani mafanikio huja baada ya kuamini anasema Lao Tzu. Kuwa mpambanaji kila Siku fanya mambo yanakuelekeza kuzishinda ndoto zako.

Hata kama umeshindwa usikate tamaa, mafanikio yako mikononi mwako. Bwana Thomas Edson alifanya majaribio 1014 kabla ya kugundua umeme wa taa zinazowaka. Je wewe umeshindwa Mara ngapi na kukata tamaa?.

Hata kama umekataliwa utapendwa pia, mafanikio yako mikononi mwako, Paul Pogba aliuzwa kwa mkopo toka Manchester United mwaka 2010, akiuzwa kwa kusema kiwango ni kidogo, Leo hii ndiye mcheza ghali duniani tena kanunuliwa na timu yake ile ile. Bw.Honda alienda kuomba kazi kwenye kampuni ya Toyota, alinyimwa kazi katika kampuni hiyo alienda na kuanza kapuni mpya ya Honda. Ni nani leo asiyeijua kampuni ya Honda Leo hii.

Ndio maana nasema mafanikio yako mikononi mwako, sijawahi sikia kuna mmama kajifungua, matatizo au mafanikio, huwa ni mvulana au msichana. La msingi ni kujiandaa kupambana na kuyafikia malengo yetu. Mafanikio yako mikononi mwako.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane;0764145476
Whatsapp; 0625951842.
Instagram: @eddybide.

Tukutane kesho kwa makala nzuri kama hii.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.