Wednesday 9 November 2016

Kusahau Ulipotoka Ni Kujiua Mwenyewe.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na safari ya kuyatafuta mafanikio. Usichoke kupambana.

Siku moja bwana Billgate alienda kwenye mgahawa na mtoto wake wa kike. Baada ya kumaliza kula mapochopocho Billgate alimpa mhudumu dola 5. Mhudumu huyo alimuangalia Billgate kwa mshangao. Billgate nae aliweza kugundua hali hiyo ya mhudumu huyo. Alimuuliza mhudumu, nini tatizo?.
Mhudumu alijibu na kusema "Nashangaa mwanao kanipa dola 500 na wewe umetoa dola 5 na mwanao ni mtoto wa tajiri namba moja duniani".
Billgate alitabasamu na kusema "Ni vizuri ni mtoto wa tajiri namba moja duniani na Mimi ni mtoto wa mkata mbao". Wapendwa kusahau ulipotoka ni kujiua mwenyewe.

Inatupasa tukumbuke yaliyopita maisha yetu ya zamani tuliyopita kwani yanatutia msukumo wa kupambana na pia kuziona Baraka za Mungu kwetu sisi. Yaliyopita ndio yaliyotuleta Leo tulipo na ndiyo yanatupeleka kesho yetu.

Uhuru tulionao Leo kuna watu walioupigania kuanzia vita vya wangoni hadi majimaji. Ndio maana tuna siku za kuwakumbuka mashujaa wetu na kusherehekea siku za uhuru.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo wahenga walisema tukumbuke pia mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kumbe Leo ndio kesho ya Jana. Tucheze vizuri na wakati wa Leo kwani nao utapita tu.

Yaliyopita pia yanatuonesha ni hatua gani tumefikia, tumekua kiuchumi, kisaikolojia, kielimu, kidini na kadhalika. Yaliyopita pia yanatuonesha majibu ya sala zetu kwa Mungu Leo. Mama yake Justin Bieber alipenda sana kuimba lakini hakuweza kuimba alijitahidi kumnunulia mwanae vifaa vya muziki. Leo hii mtoto wake anang'aa kimuziki. Kumbe yaliyopita ni majibu ya sala zetu na ndio chachu ya mafanikio yetu leo.

Je yaliyopita ni funzo kwako na yanakupa amasa ya kupambana?.
Kumbuka kusahau ulipotoka ni kujiua.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476
Whatsapp:0625951842.
Instagram; @eddybide
Email: ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yangu ya Facebook #bideismblog

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: