Sunday, 6 November 2016

Kushindwa Ni Vijilia Ya Kushinda.

Kukosa njia ni kujua njia. Kushindwa ni ngazi ya kupandia kuelekea kwenye ghorofa ya ushindi. Kushinda ni Giza linalotangulia mwanga wa kushinda.
Wakorea wanasema "usitishwe na kivuli, kinaonesha kwamba mwanga unakaribia".

Usikate tamaa. Fanya uwezalo. Mtu anayesema, nimefanya niwezalo si mtu atakayeshindwa. "Njia ya uhakika ya kutoshindwa ni kudhamilia kushinda", alituasa Richard Brinsley Sheridan. Penye nia pana njia.

Aliyekuwa waziri Mkuu wa Uingereza wakati wa vita Kuu ya Pili ya Dunia Churchill Winston, alipokuwa mwanafunzi wa madarasa ya chino aliposimama kuongea wanafunzi wenzake walicheka namna alivyoongea. Aliwaambia, "siku moja mtafurahia kusikiliza nikiongea". Aliinukia kuwa mwongeaji mashuhuri sana anakumbukwa sana katika hotuba aliyotoa yenye kichwa: Damu,Jasho na machozi kwa askari ili wapiganie nchi yao. Aliwaambia kuwa hana cha kuwapa, hana cha kuahidi isipokuwa, damu, jasho na machozi anayeipe nchi yake awe tayari kuipigania. Aliyeshindwa kuongea vizuri aligeuka kuwa mwongeaji bora. Kumbe kushindwa ni  vijilia ya kushinda ukitambua makosa yako na kuyatambua.

Waza kushinda. Fikiria kushinda. Ota ndoto za kushinda. Sema mazuri juu ya kushinda, "Unaweza kumgundua mtu ambaye ameshindwa kwa jinsi anavyosema vibaya juu ya kushinda".

Unaposhindwa usikate tamaa, pambana vumilia utashinda tena. Rafiki yangu Godius Rweyongeza aliwahi kuandika makala na kusema "Mlango mmoja unapofungwa milango saba inafunguliwa" Mimi naongeza kusema kwamba mlango mmoja unapofunga, milango saba na madirisha yake ufunguliwa. Hapa la msingi tusibaki kukodolea macho hule mlango uliofungwa. Tuwe na macho ya kuona iyo milango saba na madirisha vilivyofunguliwa.

Kamanda wa majeshi alijificha pangoni baada ya jeshi lake kushindwa kama alivyofanya Gaddafi. Alipokuwa pangoni alimuona mdudu akiwa amebeba chakula anajaribu kupanda jiwe. Mdudu Hugo alidondoka Mara Tisa akiwa amebeba chakula. Mara ya kumi mdudu huyo alifanikiwa kupanda jiwe. Askari Hugo alipoona mdudu huyo alivyofanikiwa alitoka nje ya pango na kurudi uwanja wa mapambano. Hoja kubwa si kushinda, hoja unashinda hoja unashinda katika nini?. "Afadhali nishindwe katika shughuli ambayo siku moja itashinda kuliko kushinda katika shughuli ambayo siku moja itashindwa,". alisema Woodraw Wilson.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476
Whatsapp; 0625951842
Instagram: @eddybide

Tukutane kesho kwenye makala nzuri kama hii.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

2 comments:

SONGA MBELE said...

keep it up����������������������������������
������

Edius Katamugora said...

Yes bro