Friday, 25 November 2016

Ukisema haiwezekani Ntakuuliza Lini

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog.
Ni matumaini yangu kuwa umeiona siku mpya salama kabisa. Hivyo basi tumshukuru Mungu kwa siku nyingine itakayotuwezesha kukua kiakili,kimwili,kiroho na kiafya. Nikushukuru pia kwa kuwa msomaji hai wa makala mbalimbali za blog hii.

Karibu katika makala ya Leo inayosema "ukisema haiwezekani ntakuuliza lini?". Huu ni msemo wa mwandishi wa kitabu cha "success is never final,failure is never end" Bw. Robert Schuller. Katika historia tunasoma kwamba wanadamu alipitia zama mbalimbali kama vile: zama za mawe mwanzo, zama za mawe kati, zama za chuma na  zama za sasa. Mwanadamu wa zama za mawe za kwanza na za kati alizoea kutumia mawe kama kifaa cha uwindaji na alizoea kula mizizi na matunda. Ilipofika zama za mawe za kati aliweza kugundua moto na alianza kula vyakula vya kuchoma na inasemekana kwamba ni wakati huu ambapo mwanadamu alianza kuishi sehemu moja yaani alijenga nyumba na alianza kufuga wanyama kama vile mbwa. Baadae alifudua chuma katika zama za mawe za kati hapa ndipo alipoanza kutengeneza mikuki, majembe na vifaa vingine vya chuma. Mwisho wa siku alifikia katika zama za sasa ndio wakati tulipo. Kumbe ukisema haiwezekani mtakuuliza lini. Mwanadamu wa zama za mwanzo hajui lolote kuhusu chuma, ufugaji,kilimo na makazi ya sehemu moja. Alizoea kutangatanga huku na huko.

Nimeanza kukumbushia historia hiyo ya ukuaji wa mwanadamu ili kuonyesha kwamba katika maisha yetu ya kila siku kuna mabadiliko yanayootokea ndio maana hatupaswi kusema jambo Fulani haliwezekani. Watu wa zamani walizoea kutembea katika njia ndogo ndogo (foot paths) baadae walianza kutembelea wanyama kama vile farasi na punda wakapanua njia na kuwa kubwa kidogo (earth roads), wakafanikiwa kutengeneza barabara za kokoto na Leo hii tunaona mpaka barabara za lami. Kuna watu wengi wamekufa kabla ya dawa mbalimbali kugundulika. Baada ya dawa kama za malaria na kipindupindu kugundulika watu wengi wamepona kupitia ugunduzi huo.

Kila kitu kinawezekana ndilo jambo ambalo tunapaswa kuweka akilini mwetu. Kuna wakati utataka kufanya kitu Fulani watu watakwambia mbona mtu Fulani alijaribu akashindwa. Usikate tamaa pambana na zidi kusonga mbele kwani kila mtu Mungu anampangia njia na uwezo wake wa kufanya vitu kiutofauti. Bw. Edson Thomas mgunduzi wa Umeme alifanya majaribio 1014 kabla ya kugundua Umeme. Huyu bwana angesema haiwezekani nadhani hadi Leo hii tungekua tunatumia vibatari, chemli na koroboi kama vyanzo vya mwanga na pia mishumaa. Michael Jordan alifukuzwa katika timu ya kikapu ya highschool alikokua akisoma alikwenda na kujifungia ndani na kulia kwa uchungu kisha alianza kufanya mazoezi makali huyu ndiye Michael Jordan tunayemfahamu sasa kama mchezaji bora wa kikapu.

Kuna msemo wa kiingereza unaosema "evrything is possible becase even the word impossible says I am possible" kila kitu kinawezekana kwa sababu hata neno haiwezekani linasema nawezekana. Kumbe kila kitu kinawezekana.Watu wa miaka ya 1910 hawajui kuhusu TV lakini wale wa miaka ya 1920 wanalijua hilo. Ndio maana mmiliki wa Microsoft bw . Billgates anasema kwamba miaka ijayo watu watakuwa na kompyuta hadi za mifukoni. Huyu anaamini katika uwezekano. Kumbe ili tufanikiwe tuweke zana vichwani mwetu kwamba kila kitu kinawezekana na tufute kabisa neno haiwezekani katika vichwa vyetu.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Eddy Bide
Tuwasiliane
Simu 0764145476
Whatsapp;0625951842
Instagram; @eddybide

Usisahau kulike page ya Facebook #bideismblog

Endelea kusoma makala nzuri katika blog hii.

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: