Tuesday, 29 November 2016

Usichokijua Kuhusu Mafanikio Yako

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog.
Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na maisha yenye kusaka mafanikio.

Leo katika Makala ningependa niongelee kiungo muhimu ambacho kitakuwezesha wewe kufanikiwa. Kiungo chenye ni Watu. Ili biashara ikue inahitaji watu, ili blog ikue inaitaji watu, ili kampuni ikue inaitaji watu wa kununua bidhaa za kampuni husika.

Kumbe watu ni kiungo muhimu katika maisha yetu ya kila siku na hasa yale yenye mafanikio. Ndio maana mtu akitaka kufunga ndoa au sherehe yoyote anapitisha michango kwa watu ili aweze kufanikisha sherehe iyo. Shule haiwezi kuwa shule kama haina wanafunzi na walimu. Kampuni haiwezi kuwa kampuni kama haina wafanyakazi, ata hii blog haiwezi kuwa blog kama haina wasomaji ambao ni watu. Kumbe kila kitu kinaitaji watu.

Mwandishi wa kitabu cha "how to be happy and influence friends" Dale Carnegie anasema ili uweze kufanikiwa jitahidi kuonesha kila mtu asa rafiki zako kwamba unawathamini. Ukimthamini mtu na yeye atakupa muda wake wa kukuthamini. Kumbe tujifunze kuwathamini watu kwani ndio chachu kubwa ya mafanikio.

Katika watu tunapata mbinu na fursa MPYA. Katika watu tunapata ushauri na katika watu tunapata  mafundisho yanatuwezesha kufanikiwa. Kuna mtu aliwahi kusema "huwa nakuwa makini pale asa ninapokutana na mtu MPYA "

Ivyo basi tujitahidi kila mara kuishi vizuri na watu kwani ni chachu kuu ya kutuletea mafanikio.

Ni  Mimi rafiki na ndugu yenu.
Eddy Bide
Tuwasiliane:0764145476
Whatsapp; 0625951842
Instagram:@eddybide

Usisahau kulike page ya Facebook #bideismblog

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: