Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri katika kuyatafuta maisha yenye heri na fanaka.
Karibu sana katika makala ya Leo inayozungumzia unavyofikiri ndivyo utakavyo kuwa.
Fikra zetu zina maana kubwa katika maisha yetu kwani zinatusaidia kufikia malengo yetu. Ukifikiria kuwa tajiri utakuwa ukifikiria kuwa maskini wa kutupwa utakuwa na kadhalika.
Fikra ni kama picha au ndoto ambazo uzunguka vichwani mwetu. Nimelala natizama filamu ni kitendawili ambacho jibu lake ni ndoto.
Kuna wakati niliwahi kuandika kuhusu kuwa na fikra chanya na nikaelezea umuhimu wake na hasa sheria ya ukiri ( kuona mambo katika fikra zetu).
Kama una ndoto ya kuwa na gari kuwa na picha ya gari unalolitaka ukutani chumbani kwako ukiamka kila siku unaliona gari ilo ukutani litakupa amasa ya kufanya kazi kwa bidii ili upate gari ilo.
Leo kwa namna ya pekee nataka nizungumzie fikra mbovu nne ambazo zinatufanya tusifanikiwe.
Mwandishi wa kitabu cha "The magic of thinking big" Bw.Schwartz anazitaja fikra hizo kuwa ni:
1. Kusema unaumwa kila Mara.
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanya mambo yao wakisingizia kuumwa. Katika kitabu cha "How I lived 365 days" cha Dr.Schindler anasema kwamba kati ya wagonjwa wanne waliolazwa katika vitanda vya hospitali 3 si wagonjwa. Bali ni wagonjwa wa msongo wa mawazo (emotionally sick). Kumbe tusijijengee kichwani hali za kuumwa umwa kwani zinatufanya tuonekane kweli wagonjwa na kushindwa kufanya mambo ya kutuendeleza. Unavyofikiri ndivyo utakavyo kuwa.
2.Sina Akili.
Ni Mara ngapi umesikia mtu anasema sina akili zitakazo niwezesha kufanya jambo Fulani. Wanafunzi wengine wanashindwa darasani kwa sababu ya kujiwekea kichwani kwamba wao ni vilaza lakini si kweli. Dunia ya leo aihitaji watu wenye akili sana inahitaji watu wenye uwezo wa kuchukua mawazo na mawazo hayo yakakuletea kitu cha maendeleo. Ndio maana leo hii watu waliofanikiwa sana hawakusoma sana sisemi hawana akili, wanaupeo na fikra kubwa sana. Kwa hiyo kisingizio cha kusema hatuna akili kisitufanye tukakwama katika maisha yetu.
3. Umri umekwenda/bado Nina umri mdogo.
Kuna watu wanashindwa kufanya mambo Fulani wakisingizia umri wao umekwenda au umri bado mdogo. Umri usiwe kikwazo cha kufanya mambo ya mafanikio. Kuna wengine wanasema bora ningeanza miaka ile hapana hujachelewa anza sasa wakati wako ndio leo na kesho yako itasema umefanya nini leo. Au kuna wengine wanaogopa kufanya jambo Fulani la kimaendeleo wakisema umri ni mdogo fatilia utakuta kuna wenzako walianza umri mdogo zaidi yako. Ujachelewa wala hujawahi anza sasa.
4.Sina Bahati.
Kuna watu wanazani mtu kufanikiwa ni bahati au wanazana vichwani mwao kwamba wamezaliwa na mikosi. Si kweli kabisa hakuna watu wanaozaliwa na bahati au mikosi. Watu walifanikiwa Mara nyingi wamekumbana na misukosuko mingi wameanguka Mara nyingi wakasimama Wajapani wanasema "Anguka Mara saba inuka Mara nane" . Kumbe tusiwe vichwani mwetu kwamba hatuna bahati tupambane kuyatafuta mafanikio.
Ni malizie kwa kusema ukijenga fikra hasi kichwani mwako utabaki kuwa na maisha hasi siku zote.
Ni mimi rafiki na ndugu yenu Eddy Bide.
Tuwasiliane;0764541476
Whatsapp; 0625951842
Instagram: @eddybide
Email; ekatamugora@gmail.com
"See you at the top".
0 comments:
Post a Comment