Tuesday 15 November 2016

Jinsi Ya Kupata Wazo La Biashara Linaloweza Kukutajirisha.

Habari ndugu na rafiki mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini   yangu unaendelea unaendelea vizuri na michakato ya maisha.

Napenda kuendeleza makala niliyoanza jana. Jambo la kwanza tuliona ni kuanza na familia yako. Karibu katika mwendelezo wa makala hizi.

Jambo la pili ni; Kupitia Kusafiri.
Siri mojawapo ambayo watu hawaifahamu Leo hii ni kwamba unaweza kupata wazo kwa njia ya kusafiri. Kwa mfano wewe unakaa Mbeya na ukaenda Dar es Salaam ukaona kuna biashara inafanyika Dar es Salaam ambayo haipo Mbeya na hivyo ukawa wa kwanza kuitambulisha biashara hivyo inaweza ikawa njia nyepesi na ya haraka kukutajirisha. Mfano Mimi kabla sijafika Dar es Salaam sikujua kwamba kuna watu wanauza chenji!.   Kumbe pia kusafiri kunakusaidia kujua biashara mpya na pia kujifunza namna mpya za kufanya biashara ata kama ulikuwa mfanyabiashara tayari.

Kwa hiyo jiwekee utaratibu wa kusafiri, hata kama wewe muajiriwa kila unapopata likizo usiache kusafiri maana katika kusafiri unaweza kupata mawazo mengi ya biashara.

Jambo la tatu; Kupitia vitu unavyovipenda (hobbies).
Swala la msingi la kuanza nalo ni je wewe una hobi gani/unapenda kufanya vitu gani?. Katika vitu hivyo unavyopenda kuvifanya je utaweza kugeuza kimojawapo kikawa kinakuletea fedha?.

Bw. Steve Harvey alikuwa amezoea kuwaandikia waigizaji wa vichekesho stori za kuchekesha. Alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Ford motors. Alifukuzwa kazi katika kampuni hiyo. Alirudi mtaani akiwa hajui nini cha kufanya. Siku moja mwanamke mmoja alimuasa ajiandikishe katika wale ambao wangefanya vichekesho katika club Fulani. Steve alikubaliana na mwanamke huyo na usiku huo aliweza kupata dola 50. Kilichobaki ni historia. Leo hii bw. Steve ni mchekeshaji maarufu duniani kama walivyo kina Mr. Bean na amekuwa tajiri kupitia Sanaa ya vichekesho.

Kwa hiyo jambo la kuangalia hapo usidharau jambo unalolifanya na kuona kama unapoteza muda. Hata Mimi ninavyo andika makala hizi sipotezi muda ninamalengo ya kuandika vitabu.

Umuhimu mwingine wa kufuata hobby ni kwamba utaifanya ile kazi kwa bidii sababu ni kitu ambacho unakipenda toka mwoyoni mwako.
   Kwa hiyo jambo la msingi jiulize una hobo gani?, fuata ile hobi uliyonayo, tumia hobi yako kutatua matatizo uliyonayo kibiashara..

Tukutane kesho katika mwendelezo wa makala hizi.

Ni mimi rafiki na ndugu yenu Eddy Bide.
Tuwasiliane; 0764145476
Whatsapp: 0625951842.
Instagram: @eddybide
Email: ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: