Wednesday 28 December 2016

Hiki Ndicho Kiwanda Unachokimiliki Wewe

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini kwamba unaendelea vizuri na kupambana kuelekea kule unapotamani kufika.
Tumshukuru Mungu kwa siku nzuri kama ya leo kwani ni moja ya siku muhimu sana katika maisha yetu.

Kuna msemo unasema "Mwanafunzi akiwa tayari mwalimu anakuja" nafikiri upo tayari kujifunza kile nilichokuandalia leo.

Katika makala ya leo nitaongelea kiwanda unachokimiliki wewe mwenyewe. Kiwanda hicho ni KICHWA CHAKO. Napenda kukufahamisha kwamba hiki ni kiwanda kikubwa unachomiliki zaidi ya unavyofikiria.

Soma; Jiamini jikubali utafanikiwa

Kichwa chako ni " kiwanda cha mawazo". Ni kiwanda ambacho kinashughulika muda wote kutengeneza mawazo yasiyo hesabika, yaani mamilioni ya mawazo katika siku moja.

Uzalishaji katika kiwanda chako cha mawazo unaendeshwa na mabwana wawili, mmoja ambaye tutamuita Bwana Ushindi na mwingine ni Bwana Kushindwa.
Bwana Ushindi anahusika kuzalisha mawazo chanya. Ameiva katika kuzalisha sababu kwanini unaweza, kwanini umefanikiwa, na kwanini utaweza kitu Fulani.

Mzalishaji mwingine Bwana kushindwa, anazalisha mawazo hasi, mawazo ya kukurudisha chini. Ni mtaalamu katika kuvumbua mamilioni ya sababu kwanini huwezi, kwanini u mchovu, kwanini hutaweza. Utaalamu wake umejikita hasa katika mtililiko wa mawazo kwanini hutofaulu.

Soma: Tuone chanya katika kila jambo

Baada ya kuwaona hao wazalishaji wawili tujifunze nini.?. Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kwamba muda wote bwana ushindi ndiye mzalishaji mkuu katika kiwanda chetu. Tuwe na mawazo chanya na tujitahidi kwa kila muda bwana kushinda atawale vichwani mwetu.

Nguo unazovaa, simu unayotumia, kiatu unachovaa, nyumba unayoishi, gari unalotumia, na kadhalika ni mawazo ya watu yaliyozalishwa ndani ya vichwa mbalimbali vya watu. Lakini vichwa hivyo mtendaji wake mkuu alikuwa ni bwana kushinda. Ebu jaribu kufikiria wale waliopigania Uhuru wetu wangetawaliwa na kushindwa vichwani mwao nadhani hadi leo tungekuwa koloni. Au jaribu kufikiria Bwana Edson Thomas aliyefanya majaribio elfu kumi kabla ya kugundua taa inayowaka angetawaliwa na kushindwa kichwani mwake nadhani pia hadi leo tusingekuwa na Umeme unaowaka.

Kuna msemo unasema "unakuwa kile unachokitunza kichwani mwako"
Mwalimu Wangu aliwahi kunambia " mtu pekee atakayekukataza mtu unayetaka kuwa si mtu mwingine bali ni wewe mwenyewe. Ukichaguwa kubaki kuwa hasi utakuwa muda wote na maisha hasi yakikuzunguka".

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane
0764145476
Whatsapp; 0625951892(tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja)
Email; ekatamugora@gmail.com
Instagram; @eddybide
Facebook page; bideismblog

Asante kwa kuwa msomaji wa makala zangu.unaweza kuwaalika na marafiki zako pia kuwa wasomaji. Karibu sana

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: