Tuesday 17 January 2017

Mafanikio Ni Mtazamo

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini kwamba umeamka salama. Leo ndio kesho ya jana. Ni wajibu wako kutimiza kile ulichokipanga Jana kwamba utakifanya leo ili ufanikiwe.

Karibu sana katika makala ya leo "Mafanikio Ni Mtazamo". Kuna bwana mmoja aliyezoea kuuza Maputo ya kijani, bluu, meupe, njano, mekundu na kahawia. Hata biashara yake ingekuwa mbovu vipi bwana huyo alichukua puto moja na kuliwekea upepo na baadaye kulirusha juu na kupepea. Watoto walifurahia puto ilo na hatimaye walinunua Maputo mengine na biashara iliendelea kukua. Siku moja bwana huyu mfanyabiashara wa maputo  alikuwa akitembea njiani alihisi akivutwa koti kwa nyuma aligeuka na kumuona mtoto mdogo. Mtoto Huyo alimuuliza "hivi ukirusha puto jeusi juu nalo pia litapaa?". Bwana huyu alijibu "sio rangi au puto linalopaa Bali ni kile kilichomo ndani".
Hadithi hii inatufundisha kwamba kila kitu tunachofanya kinaanzia ndani, ndio mtizamo wenyewe.

Kampuni nyingi kabla ya kujenga jengo jipya huwa wana mfano wa jengo hilo, huwa wana mtizamo na ndoto kubwa na baadae ujikuta wamekwisha jenga jengo lote kutokana na ule mfano wao.

Mwanafunzi hawezi kufanikiwa bila mtizamo?, mfanyabiashara, muuzaji,mzazi,mwajiri, mwajiriwa bila mtizamo hawawezi kufanikiwa.

MTU mmoja aliwahi kumwambia Blaise Paschal mwanafalsa wa Ufaransa hivi "natamani, ningekuwa na ubongo wako/akili zako ningekuwa mtu mzuri". Blaise naye hakusita kujibu ;"kuwa mtu mzuri nawe utakuwa na akili zangu". Mtu huyu alikuwa na msimamo hasi.

Bofya hapa kusoma: Ukisema haiwezekani nitakuuliza lini?

Wengi tumesikia stori ya Daudi na Goliathi. Akiwa na miaka 17 mchunga mbuzi, Daudi, aliwatembelea kaka zake. Kuliluwepo na pande la mtu kutoka kijiji jirani waliyemwita Goliathi, huyu alizoea kuwaonea watu. Daudi baada ya kusikia kuhusu pande hilo la mtu aliuliza. Kwanini mtu huyo asipigwe?. Ndugu zake walimjibu "huoni kwamba ni pande kubwa la mtu kulipiga", Daudi naye alijibu "hamuoni kwamba ni pande kubwa la mtu kulikosa". Kilichofata ni historia, Daudi alimpiga Goliathi kwa jiwe moja kwenye paji la uso kutoka kwenye kombeo lake. Na hatimaye Goliathi alianguka chini na kufa hapo hapo.

Wengi wetu tupo kama ndugu zake Daudi, tumejawa na mitizamo hasi. Wakina Daudi ni wachache na ndio wale tunaowaona wanafanikiwa kila kukicha.

Kampuni kubwa ambazo tunaona kila siku kukicha zinafanikiwa ni kutokana na mitizamo yao mizuri na pia mahusiano mazuri.
Mtu anaposema "siwezi kufanya kitu Fulani" inatokana na mambo mawili, kwamba hana ufahamu kuhusu kitu hicho, hivyo kampuni itachukua muda wake kumfundisha, ama hawezi kwasababu tu ya mtizamo aliouweka kichwani mwake.

Rafiki yangu Lazaro Samweli mwandishi wa kitabu cha "Nguzo tatu za maisha" aliwahi kusema "hata kama una pesa kiasi gani kama una mtizamo wa kimaskini, utabaki kuwa maskini tu'' kumbe mitizamo yetu inachangia kikubwa katika mafanikio  yetu.

"Badili mtizamo wako,UFANiKIWE". Kuwa na mitizamo chanya.

Ni Mimi ndugu na rafiki yako.
Edius Bide Katamugora.
Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp: 0625951842 (tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja".
Email: ekatamugora@gmail.com
Facebook page: bideismblog

Washirikishe na wenzako kile unachokipata hapa.(unaweza kushare kwenye magroup ya Whatsapp au Facebook). Asante

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: