Sunday 12 February 2017

Ningejua Huja Mbele Ya Safari

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni siku nyingine tena ambayo inaongeza tija katika kile tunachokitafuta ili tufanikiwe. Mtunga mashairi mmoja aliwahi kusema "hii ndiyo siku aliyoifanya bwana tushangilie na kuifurahia". Kumbe kila siku ni muhimu katika maisha yetu.

Karibu sana katika mada ya Leo "Ningejua huja mbele ya safari".

Ni ukweli usiopingka kwamba ni vigumu kufikia utimilifu wa hali ya juu sana (to achieve complete perfection). Lakini kwa mtu anayependa kitu au kazi anayoifanya atajitahidi kuwa na utimilifu wa kazi yake kwa kujitahidi kuweka umakini mkubwa, hii yote uhitaji maandalizi makubwa na kujipanga kikamilfu kwa kazi husika.

Ukipanga vizur kazi yako au shughuli yako  unayotaka kufanya unakuwa na nafasi kubwa ya kuondoa makosa na hivyo hutajikuta Ukisema 'Ningejua!!' ambayo huja badae. Hivyo matokeo mazuri ya kazi yako huja baada ya kazi kubwa na maandalzi ya kutosha basi jipange kabla ya kila kitu. 

'Ningejua' hutokana na kutofanya maandalizi ya kutosha na kutokuwa na muda wa Kutosha wa kufikiria na kujipanga. Ukijipanga vizuri na kufanya maandalzi ya kutosha 'Ningejua' itakuwa ndoto kwako au ikitokea ni kwa bahati mbaya kutokana na ukweli kwamba binadmu hatuko wakamilifu.

Kuna msamiati wa 'kuzima moto' hii ni kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha hivyo hujikuta unaifanya akili yako kuwa na mawazo finyu na wazo linalokuja kichwani hukosa kulifanyia tafakari ya kutosha (critique) inayofaa hivyo hujikuta unafanya ktu kwa upungufu na hii huonekana baada ya matokeo ya kile ulichokifanya. Mfano ni mwanfunzi katika chumba cha mtihani na dakika chache zimebaki mtihani Kuisha hujikuta kila linalokuja akilini na linaloelekea swali kuwa jibu, hii ni kwasababu ya kushindwa kutumia muda vizuri unazima moto!
Matokeo mazuri kwa Yale tunayofanya hutokana na mikakati na mipango unayojiwekea muda ukiwa bado mbichi(virgin). Hivyo huna aja na msamiati "NINGEJUA" katika kamusi ya maisha yako!.

Hivyo basi panga kila kitu kuanzia neno mpaka tendo linaloenda kufanyika ili usiishie kusema 'ningejua!'.

Tukumbukeni neno 'NINGEJUA' liko katika wakati uliopita na huwezi kurudisha nyakati nyuma kufidia kile ulichoshindwa kutimiza katika muda muafaka. 
Jipange, NINGEJUA ni gonjwa na janga kwa muda wako na mafanikio yako!!!

Makala hii imeandikwa na EVANCE MUJUNI.
0757082633/0657923679.

Tuma neno "Subscribe" kwenda namba 0625951842(whatsapp) ili niwe nakutumia makala zangu mubashara.

Usisite kuwashirikisha wenzio kile ulichokipata.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: