Saturday 4 February 2017

Kama Huwezi Kusifia Huna Sifa Za Kukosoa.

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri na michakato yako ya kila siku ili ufanikishe kile unachokitaka.
Nikushukuru pia kwa kuwa bega kwa bega katika kujifunza na kupata taarifa,wewe sio mtu wa kawaida.

Karibu sana katika makala ya Leo.

Nayajua matendo yako huwezi kuchukuliana na watu waovu. Unajua kuyapima mafundisho ya watu. Unauwezo wa kufoka na kugombana mtu anapofanya vibaya. Unajua kukaripia na kutoa michano mikali. Unajua kuonyesha wapi mtu amekosea,wapi kazi imekosewa.

Hongera sana kwa hilo lakini Nina neno juu yako kama huwezi hujawahi kusifia basi huna sifa au vigezo vyw kukosoa.

Najua ni changamoto kwako sababu umekulia kwenye jamii ambayo ukifanya vizuri hata wazazi hawakusifii au kukupongeza. Utasikia "umeongoza kati ya vilazw unajiona una akili".
Lakini punde ukifanya vibaya makofi,matusi masimango uwii na wewe unaendeleza tabia hiyo yenye mizizi katika jamii yetu.

Ni vizuri sana kukosoa,ni vizuri kumwonyesha MTU alipochemsha. Lakini kama hukuwahi msifia ni kazi sana mtu huyo kukubaliana na mkosolewa wako.

Najaribu tu kuwaza unavyojisikia vibaya unapoona mwenzako au rafiki yako anasifiwa na kupongezwa badala ya kufurahi na rafiki yako na ujifunze kwake wewe unakosoa tu.

"Waganga wa kienyeji ndio hawawezi kuwasifia waganga wenzao ukijiona huwezi kuwasifia wenzako wanapofanya vizuri basi ujue roho ya uganga inakunyemelea na ikikuingia...!!"

Wanaojua kukosoa wanajua kusifia pia. Najua wewe ni mtoto mzuri inakuwaje unafanya hivi tena. Najua jinsi ulivyomakini na kazi yako imekuwaje kimetokea hiki tena. Ni rahisi mtu unayemkosoa kukusikiliza na kukuona jinsi unavyojali kwamba unakosoa ili mambo yaende vizuri.

Kuna watu wamesoma haya washaanza kufurahi sababi hawapendi kukosolewa acha ujinga unadhani ukifanya vibaya watu watakuacha,watakukosoa tu na unapokosolewa tafakari hata kama mkosoaji hajui kukosoa,wala usipuuzie kirahisi ukosoaji wake.

Kama unaukweli huo ukosoaji fanyia kazi utaendelea kufanya vizuri hata kama mkosoaji yeye ndiyo kazi yake kukosoa bila kusifia. Na kama unapenda kusifiwa kuwa mpole ndio ukubwa huo.

Ni Mimi ndugu na rafiki yako.
Edius Bide Katamugora

(Makala hii imetoka katika kitabu cha "To Be Is To Do" cha Emmanuel Makwaya, usisite kutafuta nakala yako).

Tuwasiliane;
0764145476
Whatsapp; 0625951842 (tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja"
Email:ekatamugora@gmail.com
Facebook page: bideismblog (like page yetu).

Usisite kuwashirikisha na wenzako kile unachokipata hapa.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: