Sunday 30 April 2017


Habari mpendwa msomaji wa Makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na hupo tayari kufanya makubwa siku ya leo. Nikukumbushe ya kwamba leo ni siku muhimu usikubali kuipoteza. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya leo niliyokuandalia. Wazazi wengi wa leo hii wamekuwa wakichangia makubwa katika malezi ya watoto wao hasa katika mambo hasi. Wahenga walisema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" awakuishia hapo wakaongeza "samaki mkunje angali mbichi."
Imekua kasumba kwa baadhi ya wazazi kuona watoto wao wameanzisha tabia fulani isiyo njema na wenyewe kusema "bado ni mtoto mdogo akikua ataacha." Kumbe hawafahamu yakwamba anaweza kukua akakuta ameacha ndipo pale tunapokuja kukumbuka msemo huu "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu."

Mzazi kama mzazi ni jukumu lako kufuatilia tabia ya mwanao na kumkanya pale anapoanzisha tabia zisizo na maadili. Binafsi uwa nashangaa unapokuta mzazi kamvalisha mtoto wake nguo fupi huwa inaniumiza sana. Hivi unategemea mtoto kama huyu akifika shuleni wakamwambia avae sketi ndefu hatakubali? Hapana ni kwasababu ulimzoesha nguo fupi. Mazoea hujenga tabia. Na uchunguzi unaonesha kwamba tabia mpya huanzishwa ndani ya siku thelathini. Kumbe watoto wetu wanapoanzisha tabia Fulani ambayo haifai ndani ya siku thelathini inakuwa tabia yao ya kudumu.

Wazazi wengine wamekuwa chanzo kikuu cha kuwaangusha watoto wao. Mtoto anahitaji uaminifu mkuu toka kwa wazazi wake,inapofikia hatua mzazi aoni kesho ya mtoto wake ni hatua mbaya. Ukimuonesha mtoto kwamba unamuamini naye atakuwa tayari kupambana. Kwa mfano mzazi anayesema "mwanangu soma kwa nguvu zako zote huwe daktari,injinia,mchungaji na kadhalika na mwingine akasema "yaani wewe sijui utakuwa nani kwenye ukoo wetu hajawahi kuzaliwa mtu kama wewe." Ni sentensi mbili ambazo zinasauti za upekee. Na Bahati mbaya watu wengi wamekuwa wakiyabeba maneno yale mabaya walioambiwa na wazazi wao toka wakiwa bado wadogo hadi wamekua.

Siku moja askari magereza mmoja alikua akiwauliza wafungwa swali hili "ni nani kati yenu wazazi wenu waliwaambia mtaishia gerezani?," karibu wote walinyoosha mikono. Kumbe wazazi walikwisha watabiria watoto wao maisha ya gereza toka wakiwa uraiani.
Wazazi inapaswa mbadilike watoto wenu wafundishwe maadili bora. Msiwatabirie mabaya na kusema kwamba mtoto kaanzisha tabia Fulani, akikua ataacha unajidanganya mwenyewe. Anaweza kukua akakuta ameachwa.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
EDIUS BIDE KATAMUGORA
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: