Friday 28 April 2017

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kufanya makubwa siku ya leo. Nikukumbushe kwamba leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya leo niliyokuandalia. Kama umekuwa mfatilia mzuri wa michezo mbalimbali fainali huwa ndiyo hitimisho la mashindano ya mchezo husika. Ili ufike fainali inakupasa uwe na maandalizi makubwa upitie katika nyanja mbalimbali.

Tuchukulie kwa mfano mpira wa miguu. Ili timu iweze kuingia katika mashindano lazima, ifanye mazoezi, inunue wachezaji, iwe na kocha mzuri. Uwanjani utakutana na mengi, kuna kupata maumivu ukiwa uwanjani. Kuna rafu, kadi za njano, nyekundu na ushindani usio wa kawaida. Ama kweli kufika fainali unakuwa umepitia mengi.
Mwaka Jana tulishuhudia timu ya Leister city ya Uingereza ikichukua kombe la ligi kuu ya Uingereza. Yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo ambayo toka ianzishwe haijawai kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza. Lakini timu iyo haikuibuka hivi hivi iliweka malengo makubwa na hatimaye kutimiza ndoto zake.

"Fainali uzeeni" ni msemo niliyouchagua leo maana kuna mengi ya kujifunza katika maisha yetu ya kila siku hasa kwa sisi vijana. Umri wa ujana ni umri ambao tunapaswa kufanya maandalizi makubwa sio umri wa kuzembea. Ndiyo maana wanasema vijana ni taifa la kesho.

Ukiwa kijana ndiyo umri mzuri wa kuwekeza ni lazima uanze ukiwa na umri mdogo. Ukifika uzeeni ndipo unapofika fainali na kutwaa ubingwa kwa kupata kombe. Na kombe halitafutwi uzeeni utafutaji wake unaanza toka ukiwa kijana. Vijana inabidi tujifunze kuwekeza taratibu. Ukinunua ardhi leo baada ya miaka kumi itakuwa inauzwa bei gani? Maana ardhi inapanda bei kila siku kila kukicha. Habari nzuri ni kwamba Tanzania kuna sehemu heka moja inauzwa hadi elfu 50, habari mbaya ni kwamba vijana hatuzioni fursa hizi. Pesa zetu nyingi zinaishia kwenye kula bata na kutumia pesa zetu kwenye kubet. Ukiendelea hivi huu msemo kwako utapita kama upepo na mti wa mpapai.
Anza leo kuwekeza kidogo kidogo ufurahie fainali uzeeni. 

Juzi tu Vodacom walikuwa wakiuza hisa kwa sh 850 hii ilikuwa fursa kubwa lakini vijana wengi hatukulitilia maanani(Mimi sio mmoja wao, nimechukua hatua). Tunasubiri tukitangaziwa kwamba hisa zinauzwa tena kwa sh 1300 kwa kila hisa moja ndipo tushutuke na kutambua kwamba fursa ilitupita.

Bakhresa alianza kuijenga kampuni yake kwa muda wa miongo mitatu (miaka 30), Dangote aliwahi kusema alikuwa akinunua mfuko wa pipi na kwenda kuziuza shuleni tangu hakiwa mtoto. Leo hii ni mfanyabiashara mkubwa na tajiri namba moja Afrika. Warren Buffett ambaye amekuwa akitajwa kama mwekezaji mkubwa wa karne ya ishirini na moja, alianza kuuza pipi mlango hadi mlango toka akiwa mdogo. Leo hii ni tajiri namba 3 duniani baada ya kutoka namba mbili mwezi uliyopita nafasi iliyochukuliwa na Jeff Bezos mmiliki wa kampuni ya Amazon. Wewe kijana mwenzangu unasubiri nini?. Shtuka, fainali uzeeni.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
E-mail; ekatamugora@gmail.com

Usisite kulike page yetu ya Facebook hapa chini. Tufollow pia kwenye twitter na instagram hapa chini.
Jiunge pia na mfumo wetu wa email hapa chini.

Washirikishe na wenzako ulichojifunza.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: