Sunday 23 April 2017

Habari mpendwa msomaji wa Makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiaandaa kufanya makubwa siku ya leo. Itumie vizuri leo yako usipoteze hivi hivi. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala nzuri ya leo niliyokuandalia.
Majina ya watu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu. Kila mara unapokutanushwa na mtu jitahidi ufahamu majina yake na unapoambiwa majina hayo yatilie maanani. Asikwambie mtu watu wanapenda majina yao sana ikiwemo wewe.

Jaribu kukumbuka Siku ile ulipokutana na mtu mliyefahamiana nyuma wewe unakumbuka jina lake yeye anakwambia "samahani hivi unaitwa nani vile." Kusema ukweli utajisikia vibaya. Kumbe la kufahamu hapo ni kwamba watu wanapenda majina yao kuliko kawaida na wanayathamini. Usiishie kujua majina ya watu jua kabisa na namna yanavyotamkika, watu hawapendi majina yao yakosewe kutamkwa, hata wewe ni mmoja wako.

Kampuni ya Coca cola ni shuhuda wa ili. Baada ya kuanza kutengeneza bidhaa zenye majina ya watu mbalimbali bidhaa hizo na ubunifu huu uliioatia kampuni kubwa faida kubwa mno. Hii ni kwa sababu watu wanapenda majina yao hivyo kununua na kutumia kitu kilichoandikwa majina yao ni sawa na kuona fahari isiyokifani.

Kampuni nyingine zimeamua hadi kutumia majina ya watu maarufu ili kuuza bidhaa zao kwani watu hao wanakubalika, ni watu waliojijengea majina. Kampuni ya NIKE inatumia jina la Michael Jordan kwenye bidhaa zake na ni bidhaa zinazopendwa sana na watu.


Wengine wameanzisha makampuni na kutengeneza bidhaa zenye majina yao. Bwana Henry Ford, Honda na Toyota ni mifano tu ya watu hao. Kumbe hata wewe kama unatafuta wazo zuri la biashara lenye ubunifu angalia ni kwa namna gani utaweza kutumia majina ya watu kwenye bidhaa au kitu utakachokuwa ukiuza au kutengeneza. 

Hii ni siri kubwa nakupa leo hii.
Anza kutumia majina ya watu na kuyathamini utaona mabadiliko. Wafanyakazi, watu wote unaoishi nao na wanaokuzunguka jitahidi kuyajua majina yao na kuwaita kwa majina yao.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145475
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook na kujiunga na mfumo wetu wa email hapa chini.

Usisahau kumshirikisha na rafiki yako Makala hizi.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Somaquran said...

Big up bro. Content yako iko poa. Na template ya blog yako iko poa sana. Keep it up