Wednesday 26 April 2017

Mitandao Ya Kijamii Na Karne Ya 21


Habari mpendwa msomaji wa makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiandaa na kujiweka tayari kutimiza majukumu yako Leo. Leo ni siku muhimu usikubali kuipoteza. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya leo.

Mitandao ya kijamii imeleta mabadiliko makubwa katika karne hii tuliyomo ya 21. Tumeshuhudia kuibuka kwa mitandao mbalimbali kama Facebook, Twitter, instagram, whatsapp, Telegram, snap chat, kutaja michache.
Kuibuka kwa mitandao hii kumeleta mapinduzi makubwa katika biashara. Siku hizi ni rahisi sana kuuza na kununua kitu chochote duniani kupitia mitandao ya kijamii.

Katika karne ya 20, kutangaza biashara, TV, magazeti, redio na vipeperushi vilitumika lakini leo hii kutumia mitandao ya kijamii unaweza kuwafikia mamilioni ya watu kwenye sekunde moja tu dunia nzima.

Je watu wanaitumia vyema mitandao ya kijamii?.

Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza na kupata majibu yasiyohesabika. Ukweli ni kwamba watu bado hawajajua umuhimu wa mitandao hii hasa katika biashara. Unaweza kuta mtu amejiunga mitandao yote hii lakini yeye anaitumia kuchati na kutuweka picha mbalimbali zinazomuhusu tu. Hivi Unajua ukitumia whatsapp tu kwa kubadili dp yako kila siku kwa kuweka bidhaa unazouza tayari umetangaza biashara yako. Lakini wewe kila siku umekuwa mtu wa kuweka picha za kula bata sehemu za starehe. Unapoteza fursa hii.

Uchunguzi unaonesha kwamba, kama biashara yako haipo mtandaoni kwa muda wa miaka mitatu tambua kwamba itaharibika muda si mrefu. Kiukweli mitandao ya kijamii ni njia tosha ya kutangaza biashara zako na yenye kutumia pesa kidogo tu. Inasikitisha kuona mtu ana marafiki 5000 Facebook lakini hawajui anajishughulisha na nini. Hivi Unajua hao marafiki zako tayari ndiyo Wateja wako na bado unalalamika eti biashara haiendi sipati Wateja.

Siku moja wakati naendesha semina kuhusu vipaji niliwahi kuwaambia watu kwamba kama unakipaji kwenye kurasa za mitandao yako hakikisha unaweka mambo yanayohusu kipaji chako. Inasikitisha kuona umejaza marafiki wengi na hawajui huna kipaji gani. Ukionesha ni vitu gani ulivyonavyo ndivyo kadri sapoti kutoka kwa watu wengine inapojitokeza. Acha kuficha vipaji vyako vioneshe kwenye mitandao yako ya kijamii. Michael Jordan akiwa shule alifukuzwa kwenye timu ya kikapu kwamba hajui kucheza vizuri, alijifungia ndani na kulia na baadae aliamua kufanya mazoezi kwa bidii. Leo hii ni moja kati ya wachezaji bora wa kikapu waliowahi kuwepo katika dunia hii. Unafikiri angeendelea kulia na kujifungia chumbani hangejulikana?, hasha!.

Bwana Robert Kiyosaki aliwahi kusema " leo hii unaweza Fanya biashara kirahisi zaidi ya ilivyokuwa. Ukiwa na simu tanashati (smart phone) unaweza kuuza chochote. Kama unamiliki simu tanashati na hujawahi kuuza chochote tambua yakwamba unafanya makosa makubwa."

Kumbe inapaswa wengi tubadilike na kuitumia vyema mitandao ya kijamii. Hii ni fursa kubwa kwetu na hasa vijana tunaopenda kuwa wajasiriamali. Kwenye mitandao ya kijamii tujitahidi kuweka mambo yanayohusu biashara au shughuli zetu. Kuna msemo unasema "biashara uenda macho yanapokwenda" wengine wakaongeza "biashara ni matangazo."
Kama biashara ni matangazo na huenda macho yanakokwenda basi macho ya watu wengi siku hizi yameelekezwa kwenye simu. Watu wamelewa simu. SAA hata moja haliwezi kupita bila kuingia mitandaoni. Hawaangalii tena TV au kusikiliza redio kama ilivyokuwa nyuma, wamehamia kwenye mitandao ya kijamii. Wewe kama mfanyabiashara ni jukumu lako kuwafuata huko.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (whatsapp)
E-mail; ekatamugora@gmail.com
Instagram: @eddybide
Facebook page: Bideism Blog.

Usisite kulike page zetu za facebook na kutufuata instagram hapa chini.

Jiunge pia na mfumo wetu wa email hapa chini kwa kujaza email yako.
Usisite kuwashirikisha na marafiki zako kile unachojifunza hapa.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

Nice work Gantlemen.