Tuesday 16 May 2017

Jenga Picha (Picturization)


Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kufanya mambo makubwa siku ya Leo. Leo ni siku muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika Makala ya leo niliyokuandalia.
Mojawapo ya vitu vilivyowabadilisha wengi na kuwa na fikra za mafanikio ni kanuni ya kujenga picha(picturization).
Makampuni makubwa kabla ya kujenga jengo jipya utengeneza maboksi ambayo yanaonesha jengo litakavyokuwa. Hii ndiyo maana halisi ya kujenga picha. Kumbe tayari wanakuwa na mchoro na namna jinsi jengo lao litakavyokuwa.
Unapojenga picha kichwani mwako na kuiweka katika uhalisia unakuwa unauweka ubongo wako katika hali ya kufanya kazi ili kufikia maono ya picha yako. Kwenye Kitabu chake cha Think and grow rich, Bwana Napoleon Hill anasema "Whatever the mind can conceive, the mind can receive."
Hapa anamaanisha kwamba "kile unachokiwaza na kukiweka kwenye akili yako ndicho utakachoweza kukipata".
Kumbe tukianza kutumia kanuni hii ya picha tutafika mbali. Kwa mfano kama unataka kumiliki gari la aina
Fulani tafuta picha yake bandika maeneo mbalimbali ambako utakuwa unaliona Mara kwa Mara kwani maisha yetu yanafuata sana TASWIRA ambazo ziko Mbele yetu tunazoziangalia mara kwa mara.

Nakumbuka nikiwa kidato cha sita mwalimu Wangu wa somo la elimu kumbakumba (GS) alizoea kutwambia fumba macho na baadaye alituuliza, "fulani unaona nini?." Hapa alitaka kutujengea utamaduni wa kujenga picha.
 
Nakumbuka pia nikiwa kidato cha NNE nilibandika kikaratasi kwenye dawati langu kuhusu maksi nitakazopata kwenye mtihani wa taifa, Mungu si Athumani nilichokuwa nimekiandika ndicho nolicholipata. Kanuni hii ya kujenga picha inafanya maajabu makubwa.

Kanuni hii unapoanza kuifanyia kazi unaweza kuonekana wa tofauti sana marafiki, ndugu, wazazi wanaweza kukucheka lakini kuna msemo unasema "Fanya mambo kama kichaa."
Bandika picha kwenye sehemu maalumu kama kioo chako kwa wale wasichana wanaopenda vioo, bandika ukutani na sehemu utakapoweza kuona picha ya kitu unachotaka kukipata au kuwa. Moja wapo ya faida ya kujenga picha au kutumia kanuni hii ni kwamba kila unapoiona picha inakukumbusha kwamba kuna kitu unadaiwa hivo huna budi kuweka bidii ufanikishe ndoto zako.
"Huwezi kuzaa ndoto ambayo kwanza hujaiwazia. Lazima uiwazie ndani mwako kupitia macho ya imani kabla ya kuitoa nje. Badili kile unachokiona, utabadili kile unachokizalisha." Anasema Joel Osteen' 

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
Tuwasiliane
0764145476
0625951842 (whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini na pia kujiunga na mfumo wa email( chini kabisa utaona sehemu ya kujaza email yako) ili upate Makala hizi moja kwa moja Mara tu zinapowekwa kwenye blog yetu.

Washirikishe na wenzako ilichojifunza.

See You at the top

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: