Thursday 18 May 2017

Barua Ya Wazi Kwa Wanafunzi Wote

Habari za asubuhi mpendwa mwanafunzi. Pole na masomo na shughuli zote unazozifanya.
Nimeamua kukuandikia barua hii kukupa tahadhari na kukukumbusha mambo machache ambayo ulikuwa uyajui lakini unatakiwa uyajue
                                                          

Mfumo wetu wa elimu umekuwa ni mfumo unaosisitiza vijana kujiajili lakini haumpi kijana elimu na jinsi ya kujiajili. Yaani unapewa samaki na kumla siku moja lakini haufundishi namna ya kuvua samaki, jambo ambalo lingekusaidia kuwapata samaki wengi zaidi lakini unapewa samaki mmoja ukimla kazi imekwisha. Siko hapa kuilaumu serikali hii ni barua ya wazi kwako wewe mwanafunzi.
Ukiwa chuoni utajifunza namna ya kufanya kazi fulani moja labda ualimu, uhandisi, udaktati, uanasheria, uafisa ugavi na kazi nyinginezo. Hii inaitwa specialization. Lakini kiukweli unatakiwa ujue mambo mengi zaidi ya hayo.

Unatakiwa ujue mambo mengine kama, biashara, ujasiriamali, namna ya kuishi watu na uongozi. Aya ni mambo hatujifunzi shuleni lakini unapoingia kazini unatakiwa uyajue na kama unayajua utakuwa umejiweka katika wakati mzuri wa kujiajili au kuajiliwa.

Ndiyo maana nikasema, unapewa samaki lakini ufundishwi kuvua samaki.
Je unapataje kujifunza mambo haya?.
Mambo hayo yote niliyoyataja hapo juu tayari yameandikwa kwenye vitabu na ni jukumu lako kuvitafuta kujifunza. Wanafunzi wengi hawapendi kusoma Vitabu vilivyo nje ya madarasa yao lakini ukifatilia watu wengi waliofanikiwa ni wasomaji wazuri wa Vitabu.
Katika kitabu changu kinachoitwa Barabara ya mafanikio kuna mahali nimeandika elimu peke yake haitoshi na nimeorodhesha na kuweka wazi mambo yaliyo nje ya elimu ambayo unatakiwa wewe kama mwanafunzi unatakiwa uyafahamu.

Mwingine anategemea kufanya kazi Fulani lakini hajawahi hata kununua gazeti linalotoa tangazo kuhusu kazi anayoipenda. Hajui mtu au watu wa kazi Fulani wanahitaji vigezo fulani anasubiri siku akimaliza chuo ndipo aanze kufatilia. Umechelewa ndugu yangu.

Elimu ya biashara uongozi na watu ni elimu muhimu sana. Watu wengi walishangaa baada ya Bwana Donald Trump kupata uraisi wa Marekani lakini hawajui yakwamba yeye ni kiongozi mzuri na anajua kuishi na watu. Sio Mimi ninayesema Vitabu vilikwisha kuandika kabla hata hajaanza kugombea.

Elimu kwa kifupi maana yake ni kuwa na taarifa (having information). Kama huna taarifa Fulani inamaana huna elimu. Ukiwa mwandisi unaweza kuchaguliwa labda kuwa injinia wa wilaya au mkoa. Hapa kinachoitajika ni kuwa Unajua uongozi sio kujua tu elimu kuhusu unandisi. Nafikiri umenielewa. Au una ndoto za kuwa na kampuni katika kazi unayoisomea, kama huna taarifa kuhusu uongozi jiandae kuona kampuni yako haindelei. 

Elimu ni taarifa jitahidi utafute taarifa sahii, jitahidi utafute maarifa yatakayokusaidia nje ya kazi unayoisomea.

See you at the top
Ndimi
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker.
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza hapa.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: