Monday 22 May 2017

Tuone Fursa Katika Matatizo

Bwana Thomas Edson ambaye ndiye mgunduzi wa Umeme (father of electricity) akiwa kwenye umri wa katikati ya miaka 60 alishuhudia kwa macho yake kiwanda chake alichokuwa akifanyia uvumbuzi na ugunduzi mkubwa sana kama wa kugundua taa inayowaka ambayo wanasayansi walitumia zaidi ya miaka 50 kuigundua lakini wakashindwa, yeye ambaye akusoma aliweza jambo ili ndani ya miaka mitatu. Bwana Edson alishuhudia kiwanda chake kikiteketea kwa moto na kazi zake zote zikiishia hewani kama moshi. Akiwa amekwisha zeeka sio tena kijana lilikua pigo kubwa sana kwake kwani alipoteza kitu kikubwa sana.

Baada ya tukio hilo Bwana *Thomas Edson* aliwaambia wenzake maneno haya "Mungu ameamua kuyafuta makosa yetu na kutupa nafasi ya kufanya vyema zaidi." Ni hali ya kushangaza lakini lilitokea. Bwana Thomas aliona chanya katika matatizo.

Baada ya wiki tatu kupita Thomas aligundua Kamera ni mtu wa namna iliyoje?. Ni mtu aliyeona fursa katika matatizo. Na kwenye matatizo inatupaswa tuwe watu wa kuona fursa. Baada ya watu kulalamika mvua na jua kuna aliyeona fursa akatengeneza mwavuli.

Kuna kampuni moja iliyokuwa ikitengeneza Viatu, iliwatuma watu wawili wakafanye uchunguzi kama watu wa kisiwa Fulani wanahitaji Viatu. Mtu wa kwanza alirudi na kusema "msilete Viatu watu wa huku hata hawavai viatu.". Na yule wa pili alirudi na kusema "leteni makontena ya Viatu kuna soko kubwa la Viatu huku kisiwani."
*kwenye matatizo kuna fursa nyingi zimejificha*
*kwenye matatizo usiwe sehemu ya walalamikaji kuwa na jicho la pekee la kuziona fursa*

Kwenye Kitabu changu cha *Barabara Ya Mafanikio* nimeandika "fursa haziji zikiwa na muhuri wa thamani zake" na "mlango wa fursa hauna alama ya *vuta* au *sukuma*".
*see you at the top*
Please share
Ndimi
*Edius Katamugora*
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
KARIBU SANA KUWEKA ODA YA KITABU CHA *Barabara Ya Mafanikio*
Www.Bideism.blogspot.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: