Friday 19 May 2017

Kubali Kuwa Duduwasha

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako siku ya Leo. Nikumbushe tu yakwamba, Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala nzuri sana niliyokuandalia leo hii.
Duduwasha(caterpillar) ni hatua katika hatua mojawapo ya ukuaji wa kipepeo. Kila kipepeo lazima apitie katika hatua hii ya ukuaji. Duduwasha pia ni mdudu asiyependeka na akipita kwenye mwili wa mwanadamu huleta muwasho.
                                                   

Katika maisha yetu ya kutafuta mafanikio, kuna hatua ambayo tunapitia ambayo ni sawa na kuwa na maisha ya duduwasha. Katika hatua hii ni sehemu ambayo imejaa hali ngumu na matatizo makubwa.
Kila mtu anayependa kupata mafanikio ni lazima akubali kupita katika hali hii. Hii ni hatua ya chini sana lakini ni hatua muhimu katika kuyatafuta mafanikio. "Wanaanza kwa kutambaa" ni msemo wa Kiafrika. Ili uweze kukimbia lazima upitie katika hatua ya kutambaa. Uwezi kuzaliwa wakati huo na kuanza kukimbia, hizo ni hadithi za Kirikuu.

Watu wengi hawakubaliani na hatua ngumu hawakubali kuishi maisha yenye wakati mgumu lakini wanapenda kuwa vipepeo. Hizo ni sawa na ndoto za Abunuasi. Katika Kitabu changu kinachoitwa Barabara ya mafanikio kitakachotoka mwezi ujao, kuna sehemu nimeelezea kwamba mafanikio sio bahati. Watu wengi baada ya kupita kwenye misukosuko na baadaye kufanikiwa wengine uiita bahati. Utasikia "alifanya hivi na hivi akafanikio" lakini hawajui ni kwa namna gani au maisha gani mtu halipitia.

Bwana Robert Schuller mchungaji na mwandishi wa Vitabu kutoka Marekani aliwahi kuandika Kitabu na kukipaji jina "Nyakati ngumu hazidumu, lakini watu wagumu wanadumu." Watu wanaokubali kuishi katika nyakati ngumu ndio wanaofanikiwa.

Katika kuishi maisha ya duduwasha ndipo mtu anatakiwa kulipa gharama lakini watu wengi hawako tayari kulipa gharama (nimeeongelea swala ili pia katika Kitabu Changu).
Kumbuka ili uwe kipepeo mzuri anayevutia lazima upitie katika maisha ya duduwasha. Aliko Dangote ambaye ni tajiri namba moja Afrika aliwahi kusema "Success is not a thing to achieve overnight" hapa anamaanisha kwamba "mafanikio sio kitu cha kupata kwa usiku mmoja yaani ulale uamke umefanikiwa". Kubali kuishi maisha ya duduwasha ili baadaye uwe kipepeo mzuri anayevutia.

See you at the top
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
email: ekatamugora@gmail.com

Usisite kulike page yetu ya Facebook hapa chini na pia kujiunga na mfumo wetu wa email hapa chini ili upate makala hizi kila siku.

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza hapa.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: