Monday 19 June 2017

Acha Ushabiki, Ingia Uwanjani Ucheze

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka Salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu pia kwa siku nzuri kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow. 

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia,  ili tuendelee kujifunza kitu kipya.

Kama umekuwa mfatiliaji mzuri wa michezo mbalimbali,  kama shabiki umekuwa ukikereketwa mara nyingi kutoa  sapoti kubwa pale timu yako inapokuwa uwanjani.
Unaweza kuwajua wachezaji wote, wanaocheza siku hiyo hadi makocha wao na hata benchi la ufundi kwa mchezo wa mpira wa miguu. 

Yaani kwa ufupi unajua kila kitu kuhusu timu yako unayoipenda, ambayo mtu akianza kuiponda hupo tayari siku nzima kubishania kuhakikisha unashinda. 

Umekwenda mbali zaidi na kuchukua kadi na kuwa mwanachama anayetambulika na timu. Wewe ni shabiki wa kweli. 

Timu yako inapokuwa uwanjani, unakuwa tayari kuona makosa yote na hupo tayari kusema mchezaji gani analeta uzembe uwanjani ambaye hajitumi. Mkifungwa, unajua kosa limetokea wapi na chanzo cha kufungwa kwenu ni kipi. 

Maisha yetu yapo kama nilivyoelezea hapo juu, wengi wetu ni mashabiki na sio wachezaji au makocha. 

Wengi wetu tunaona kila kitu ni chepesi na hakitumii nguvu nyingi yaani unaingia uwanjani na kufunga tena magoli matatu ya hat trick na hatimaye kuondoka na mpira
.
Ukiambiwa Fulani alifanya kitu fulani akafanikiwa, unafikiri hakutumia nguvu nyingi unafikiri mafanikio yamekuja Kama spidi ya mwanga. Unajidanganya mwenyewe, huo ni ushabiki, inakubidi uuache uanze kufanya kama wachezaji. 

Tuchukulie kwa mfano mpira wa miguu, shabiki anaona goli ni kubwa kiasi kwamba akipewa mpira apige kwake kupata goli ni jambo la kawaida. Lakini uwanjani kuna mambo mengi, kuna maadui wa timu pinzani ambao hawataki kuona unashinda na hivyo wanakukaba kwa nguvu zote. Kuna rafu na mambo mengine mengi. Hii ndiyo hali halisi ndani ya uwanja ambayo wengine hawaioni, wanasubiri tuu goli lifungwe washangilie. 

Kuna wakati watu watakuja na kukuelezea biashara fulani ni nzuri na ukifanya hivi tuu kidogo wewe ni bilionea, unaanza kuona umezungukwa na mapesa na maisha fulani ya kitajiri. Anza sasa hiyo biashara ndipo utakapoona kwamba biashara hiyo siyo ya kizembe kama ulivyoiona mwanzoni.
Kumbe kila jambo ambalo tunataka lituletee mafanikio, inabidi tuache ushabiki na kuanza kujifanya wachezaji. 

Moja wapo kati ya matajiri  mabilionea waliowahi kutokea dunia ni Bwana Henry Ford. Yeye kabla ya kumpa ajila mfanyakazi mpya alienda naye kula chakula cha mchana. Kama mfanyakazi aliweka chumvi kwenye chakula kabla ya kukionja, mtu huyo tayari alikwisha kosa nafasi ya kazi katika kampuni yake, maana angekuwa mtu wa kuchukua maamuzi bila ya kuyafanyia majaribio.

Hivyo na wewe ndugu yangu  kama ni shabiki nakushauri uache Leo, anza kucheza. Kuwa mchezaji. Maisha hayahitaji ushabiki, maisha yanahitaji uchezaji.

Mafanikio yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog).

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: