Tuesday 20 June 2017

Huyu Ndiye Mwenye Wazo La Kufanikiwa Haraka

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka Salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu pia kwa siku nzuri kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia,  ili tuendelee kujifunza kitu kipya.

Kutokana na uchunguzi uliofanyika, takwimu zinaonesha kwamba makampuni makubwa ambayo uanza kwa mawazo yao yenyewe ni kuanzia asilimia 16-20%. 

Kumbe asilimia 80% zilizobaki ni mawazo yalioyoanzishwa na watu wa kawaida sana watu ambao ni sawa na wewe.

Kumbe mawazo mazuri yenye mafanikio ya haraka unayo wewe sio mtu mwingine. 

Mark Zuckerberg mwanzilishi wa Facebook alianza akiwa bado anasoma chuo, mwaka 2004 alianzisha mtandao wa facebook ambao umemfanya kuwa miongoni mwa matajiri kumi wa dunia akishika namba sita. Leo hii anamiliki pia mitandao ya Whatsapp na Instagram. 

Salim Bhakhresa alianzia huko Zanzibar akiwa na umri wa miaka 16 alikuwa akiuza kwenye mgahawa wa chakula. Leo hii ni mtu mwingine anayemiliki kampuni kubwa ya kimataifa inayoitwa Azam. 

Kumbe hata wewe unaweza kuwa na wazo zuri linaloweza kufanikiwa kwa hali ya juu kabisa.
Jiulize Leo maswali haya:
==> Ni mambo gani napendelea kuyafanya?
==> Ni vipaji gani ambavyo ninavyo ninavyopaswa kuvitumia?
==> Ni mambo gani naweza kuyafanya kwa kujitolea bila kulipwa chochote?
==> Ni ujuzi gani niliokuwa nao ambao nimeacha kuutumia na napaswa kuanza kuutumia tena?
==> Ni ujuzi gani mpya naweza kujifunza?
==> Ni huduma gani naweza kuitoa kwenye jamii yangu na nikainufaisha jamii inayonizunguka pamoja na mimi pia?

==> Ni vitu gani navifanya inafikia wakati nasahau hata  kula?

Hayo ni maswali baadhi niliyoyaorodhesha ambayo yanaweza kukupa wazo zuri litakalo kuletea mafanikio ya haraka Sana. 

Mafanikio yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog). 

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: