Thursday 15 June 2017

Aina Mbili (2) Za Uwekezaji Unaotakiwa Kuufanya

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka Salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu pia kwa siku nzuri kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia,  ili tuendelee kukifunza kitu kipya.

Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni uwekezaji hupi ambao wanaweza kuwekeza na ukawapa mafanikio makubwa sana na mafanikio wanayoyatamani.

Leo nataka nikufundishe aina mbili za uwekezaji muhimu ambao utakufikisha kwenye mafanikio haraka sana.

Nisikupotezee muda sana karibu twende kuuona ni uwekezaji wa aina fulani unaohuhitaji:

(1). Uwekezaji wa Akili
Huu ndio uwekezaji muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu. Ukitaka kupata mafanikio ya haraka jiingize katika uwekezaji wa akili au uwekezaji wa kuikuza akili(improving mind).

Uwekezaji huu unaweza kuupata kwa kutafuta maarifa ambayo yatakusaidia kuweza kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.
Jifunze kuwekeza katika akili yako kwa kusoma vitabu vitakatifu kama Biblia na Kurani na vile vitabu vya ziada. Hakuna umaskini kwa mtu anayewekeza katika Aikili.

Kujifunza hakuishi ndiyo maana nakushauri uanze kusoma na kujifunza kila siku. Unapoanza kusoma vitabu, utaona mabadiliko makubwa na utakuwa mtu wa pekee.

Hivi unafahamu kwamba Bill Gates ambaye ni tajiri namba moja duniani huchukua likizo ya wiki moja kila mwaka ambapo anaenda mahali kusoma vitabu ili kujiongezea maarifa na namna ya kuiendeleza kampuni yake ya Microsoft. Kama Bill Gates ameweza kwanini wewe usiweze?.

Kwenye kuikuza na kuijenga akili ndiyo maana nimekuandikia kitabu changu ninachokiita Barabara Ya Mafanikio. Usisite kuweka oda yako.

2) Uwekezaji Katika Watu.
Hakuna kitu ambacho utakifanya kisicho wahusisha watu. Kumbe uwekezaji mwingine muhimu ni ule wa kuwekeza katika watu. Baada ya Dale Carnegie kutafuta uchunguzi kabla ya kuandika kitabu chake cha "How to influence people and win friends" alipata majibu kwamba watu wanapenda kusikia namna ya kuishi vizuri na watu.

Jifunze kuishi vizuri na watu kila mahali ulipo. Jenga mahusiano mema na watu wote unaokuzunguka. Watendee mema watu wote unaokutana nao kila siku. Wafanyie watu jinsi unavyotaka kufanyiwa.

Ukiwekeza katika watu kila kitu utakachokifanya kitafana, watu wanapenda kujaliwa hivyo ukiwajali tayari unakuwa umewateka. Kumbe hata ukianzisha biashara watakuja kununua kwako tu sababu unawajali, unawapenda na umewekeza kwao.

Mmoja wa watu Muhimu kwa raisi Wa Marekani Bwana Donald Trump ni mwandishi mashuhuri Robert Kiyosaki. Urafiki wa Trump na Kiyosaki umemfanya Trump kufanya vyema katika maswala ya biashara ya uwekezaji wa  majengo na uwekezaji wa viwanja vya mpira wa kete( gofu) ambavyo ndivyo viwanja ghali duniani. Hii ni kwa sababu Kiyosaki ni mtaalam sana katika maswala ya Biashara.

Jifunze kuwekeza katika watu itakusaidia na  utafanikiwa.

See you at the top

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Karibu kuweka oda ya kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kupitia mawasiliano hapo juu.

Washirikishe na wenzako kile unachojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

Mwenyezi akutangulie....