Wednesday 14 June 2017

Huyu Ndiye Adui Mkubwa Anayekusumbua

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka Salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu pia kwa siku nzuri kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia,  ili tuendelee kukifunza kitu kipya.

Watu wengi wameshindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu ya uadui waliojijengea ndani mwao. Kiukweli adui namba moja wa wewe kutokufanikiwa ni wewe mwenyewe.

Wakati mwingine utasikia mtu akimlalamikia mtu Fulani kwa kusababisha kutofanikiwa kwake, lakini anasahau kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyechangia makubwa ili asifanikiwe.

Wengine wamekuwa wakilaumu kwa jazba kuzaliwa kwenye familia duni lakini Bill Gates ambaye ni tajiri namba moja anawajibu akisema "Kuzaliwa maskini sio kosa lako, kosa lako ni kufa ukiwa maskini."

Kumbe wewe ndiye adui wa kwanza wa mafanikio yako tukiachana na maadui WA nje.

Wengi tumejijengeea maadui wengi ambao wanasababisha tusifanikiwe.  Umejijengea mtizamo hasi ndiyo maana haufanikiwi. Umejijengea hofu inayokusababisha ukose uthubutu wa kufanya mambo makubwa.

Umeweka hofu kichwani mwako hutaki lioness kipaji au vipaji ulivyojaliwa.

Umejijengea hofu ya "watu watanisemaje", ndiyo maana unashindwa kufanya mambo makubwa.

Kuna methali ya Kiafrika inasema "Kama huna adui wa ndani, adui wa nje awezi kukuletea madhara yeyote."
Kumbe maadui tunao sisi wenyewe ndani yetu.

Siku moja wakati namsikiliza mhamasishaji toka Marekani Bwana Les Brown  aliwahi kusema, ukienda makaburini utakutana na mambo ya kusikitisha, utakutana na vitabu ambavyo havijawahi kuandikwa, utakutana na vipaji ambavyo havijawahi kuonekana, utakutana na mawazo mazuri ya biashara ambayo hayajawahi kuvumbuliwa.  Watu wamekufa wakiwa na mambo makubwa lakini maadui waliokuwa ndani mwao wamesababisha wasifanye makubwa.

Adui yako namba moja ni wewe mwenyewe.

See you at the top

Ndimi
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476/0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.

Karibu Sana kuweka oda ya kitabu cha "Barabara Ya Mafanikio"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: