Thursday 29 June 2017

MAMBO 21 NILIYOJIFUNZA MIAKA KADHAA ILIYOPITA



Kuwa na hisia za kutoa shukrani bila kuzitoa ni kama kuandika barua bila kuituma. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha leo hii kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa. Nawashukuru pia wazazi wangu na nawaombea daima kwa Mungu awazidishie Zaidi na Zaidi. Nawashukuru pia kwa malezi na elimu bora waliyonipatia. Mungu awabariki.


Aidha namshukuru kila mmoja aliyechangia kwa namna moja ama nyingine kunifanya leo nimekuwa hivi nilivyo. Ni kwa neema tu.

Leo mpendwa msomaji ningependa nikushirikishe mambo 21 muhimu ambayo nimejifunza miaka kadhaa iliyopita.

Mambo hayo, baadhi ni sehemu ya maisha yangu, mengine nimejifunza kutoka kwenye mazingira niyokulia na niliyowahi kuishi na ninayoishi, watu niliyokutana nao kwenye maisha yangu, vitabu nilivyosoma, kutaja machache.

 Mambo hayo 21 ni kama yafuatayo:

1)       Sala na Imani ni vitu muhimu kwenye maisha ya mwanadamu yeyote. Kila siku kumbuka kumshukuru Mungu na kumuomba Zaidi na Zaidi. Usiifanye sala kama spea tairi, unapopatwa na matatizo na majanga ndipo unapokumbuka uwepo wa Mungu. Imani ni kama mswaki,utumie kila siku, lakini usitumie wa mtu mwingine.

2)      Ipende familia yako na ndiyo iwe mstari wa mbele kwako. Kama umezaliwa katika familia duni, kubaliana na hiyo hali kama chagamoto na pambana kuhakikisha familia yako inaendelea.

3)      Ukitumia kipaji chako utafanikiwa kwa haraka sana kama ukiamua. Kipaji ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliyenacho, kila kigeukapo ufanikiwa. Kila mtu anapozaliwa anazaliwa na vipaji na uwezo kuanzia 500-700, cha ajabu kuna wengine bado hawajatambua na kuanza kutumia vipaji walivyojaliwa. Kuna msemo unasema “Kila mtu amezawadiwa lakini kuna watu hawajawahi kufungua maboksi ya zawadi zao.”

4)      Kila siku kwako itakuwa kama siku ya Valentine kama utakuwa kwenye mahusiano na mtu sahihi(everyday will be Valentine, if you are with the right person.)

5)      Marafiki unaoambatana nao kila siku watakusaidia ufanikiwe au watakusaidia usifanikiwe. Chagua na ambatana na marafiki sahihi. Tabia za marafiki zako zinamchango mkubwa kwenye tabia yako. Niambie rafiki yako, nikwambie tabia yako.

6)      Ukiwekeza katika kusoma vitabu na kutafuta maarifa mbalimbali, utaweza kujiingizia kitabu kwa urahisi sana, kwani ni watu wachache wanafanya hivyo.

7)      Kuandika kitabu ni alama tosha itakayodumu vizazi na vizazi.
8)      Unachokijua wewe, kuna watu wengi hawakijui, hivyo ni vizuri kuwashirikisha ili wajifunze na kufanikiwa. Pia utaweza kujiingizia kipato kwa kutoa ujuzi ulionao.

9)      Kila unayekutana naye una mengi ya kujifunza kutoka kwake. Kuwa mwangalifu kila unapokutana na mtu mpya.

10)  Kutoa ni moyo vidole uachia. Ukitoa upendo na ukarimu kwa watu wote wanaokuzunguka, utapokea upendo na ukarimu kutoka kwa watu hao pia. Utavuna ulichopanda.

11)  Elimu ya darasani haitoshi ukiishia kusoma uliyojifunza darasani. Unahitaji kwenda hatua Zaidi na kutafuta maarifa Zaidi.

12)  Elimu yako haipaswi kukutenganisha na jamii inayokuzunguka, kama ukijitoa kwenye jamii uliyokuwa ukiishi tambua elimu yako haijakusaidia.

13)  Fursa zipo mahali popote ulipo, huhitaji kwenda mbali na mahali ulipo kuzitafuta. Mafanikio yapo mikononi mwako. Dig gold where you are.

14)  Malezi bora ya wazazi yanamchango mkubwa katika maisha na mafanikio ya watoto wao. Umri mzuri wa kumfundisha mwanao ni kuanzia pale anapozaliwa hadi anapotimiza miaka 12. Samaki mkunje angali mbichi.

15)  Huhitaji umri mkubwa kufanya mambo makubwa nay a ajabu. Watu wengi waliofanikiwa walianza wakiwa wadogo.

16)  Mitandao ya kijamii itakusaidia kujulikana kwa haraka sana na pia kutengeneza branda yako( jinsi unavyojenga picha vichwani mwa watu pale unapotajwa.) kwa muda mfupi na kwa kutumia gharama ndogo sana.

17)  Umaskini wa mtu unaanzia kichwani kwake, sio kukosa mali tu ni mwa kuwa na mtizamo hasi aliyojijengea ndani mwake. Kumbuka pia pesa ni mtumwa, wewe ni mfalme. Usibadili fomula hiyo kwenye maisha yako.

18)  Uvumilivu na subira ni kitu muhimu san hasa kwenye kuanza kuonesha vitu ulivyojaliwa navyo kama kipaji na ujuzi ulionao n ahata kwenye kufanya biashara. Kumbuka unachokitafuta kinakutafuta (kanuni ya uvutano), hivyo ni wajibu wako kukitengenezea mazingira sahihi ili kije kwako. Juhudi, bidii na kujituma view nguzo kuu kwako.

19)  Ukibadilika kila kitu kwenye maisha yako kitabadilika.

20)  Muda ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu. Ukitambua umuhimu wa muda na kufanya mambo kuendana na muda utafaikiwa. Habari mbaya ni kwamba muda unapaa, habari nzuri ni kwamba wewe ni rubani. Kila siku ni muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.

21)  Ulipozaliwa ulikuja duniani ukilia huku dunia ikishangilia. Ni wajibu wako mkubwa kubadili kile kilichotokea wakati unazaliwa pale unapoiaga dunia, yaani unapoiga dunia, wewe unashangilia na dunia inauzunika kwa sikitiko kuu. Mambo haya yote utayafanya kwa kutimiza kusudi lako. Anza kwa kujiuliza ulikuja duniani kufanya nini? Kumbuka, Mungu alikuumba ili uje duniani kutimiza kusudi Fulani. Hakuna aliyezaliwa kwa bahati mbaya. Hakuna aliyekuja duniani kuzurula na kusindikiza wengine.

Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
Author and motivational speaker.
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

washirikishe wenzako ulichojifunza.

kTangazo: Kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO kinaanza kuuzwa rasmi kesho, kwa wale walioweka oda kama unahitaji kitabu hicho karibu kuweka oda kwa mawasiliano hapo juu. Bei ni shilingi  6000, baada ya wiki 2 bei itakuwa 10000.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: