Wednesday 28 June 2017

Mambo II Yanayokusababisha Usianze Kitu Unachotaka Kuanza

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima na mwenye afya tele. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana tuweze kujifunza kitu kipya kitakachoweza kuchangia katika kuyafikia mafanikio yetu.
Leo ningependa ujifunze mambo mawili yanayokusababisha wewe kutokuanza kupambana kufikia ndoto au malengo yako
.
Mambo hayo mawili ni haya yafuatayo:

1) Ukamilifu (perfectionism):
Watu wengi wameshindwa kuanza kwa sababu tu wanasubiri ile hali ya utimilifu katika kile anachotaka kukifanya. Kama anataka kuanza kufanya biashara fulani anasubiri afikishe labda milioni 5 ndiyo aanze biashara. Anasahau kwamba biashara inaanza kufanyika kwa mtaji kidogo.

Kama anataka kuwa mwandishi wa vitabu au makala mbalimbali, mtu huyo anataka aandike kitabu kizuri kisicho na kosa hata moja ndani yake. Ndiyo maana kuna chapa ya pili na ya tatu ili makosa 
 yafanyiwe marekebisho.

Ndugu msomaji kama na wewe hupo katika kundi ili la watu wanaotafuta utimilifu, unachelewa sana.
Amka kutoka katika kitanda cha kutafuta utimilifu, anza kufanya taratibu ukamilifu utaupata huko.

Nakubaliana na Paul Arden aliyewahi kisema "Badala ya kuutafuta ukamilifu, anza kufanya unachotaka kukifanya, ukamilifu utautengeneza njiani. "

Wengine wakaenda mbali zaidi na kusema "Hakuna aliye kamilika ndiyo maana hata penseli zina vifutio. "

Usisubiri ukamilike kwa kila kitu anza taratibu mambo mengine yatajileta mbeleni.

2)Uvivu:
Uvivu ni chachu kubwa inayowapelekea watu wengi kushindwa katika mipango yao na pia katika malengo yao. Watu wengi wanashindwa kutumia vipaji vyao sio tu kwamba hawawezi kuvimudu vyema, la hasha. Ni kwa sababu tu wamejijengea uvivu ndani mwao.

Uvivu ni adui mkubwa wa maendeleo ya mtu na pia ni adui wa mafanikio. "Uvivu ni tabia ya kupumzika kabla haujachoka. " anasema Jules Renard

Acha uvivu leo anza kufanya kile ulichopanga kukifanya kwani una uwezo mkubwa wa kukifanya amka toka kwenye kitanda cha uvivu, nenda kapambane na utafanikiwa.

Mwisho wa siku nikutane na wewe ukinena maneno haya "itakuwa inatisha sana nisipotumia uwezo wowote niliyo nao. Ningetishwa sana na kuhairisha na uvivu." kama anavyosema "Denzel Washington

Mafiniko yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora 
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog). 

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: