Saturday 17 June 2017

Matatizo ni Mtihani, Kubali Kuufanya

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka Salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu pia kwa siku nzuri kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow. 


Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia,  ili tuendelee kujifunza kitu kipya.

"Kiletacho njaa ndicho kitakachokuonesha chakula kitokapo. " ni msemo wa Kiafrika.
Leo wakati naamka nimejaribu kutafakari na kumkumbuka mwalimu mmoja wa somo la hisabati (Advanced Mathematics)  aliyekuwa akifundisha kidato cha tano na sita. Kwenye mazoezi yake aliyoyatoa darasani aliandika neno "problems" akimaanisha "matatizo", yaani  kila swali ambalo yeye alilitoa kwa wanafunzi wake lilikuwa ni tatizo lazima litafutiwe ufumbuzi.

Maisha yenyewe hivyo hivyo yamejaa matatizo mengi ambayo ni mitihani inayopaswa kufanyika na mtu kufaulu.

"Kulikuwa na mtu mmoja pande la mtu aliyekuwa mbabe sana akiwaonea watu wa kijiji fulani. Pande ili la mtu liliitwa Goliathi, baadaye alijitokeza kijana mdogo na kusema kwamba atapigana naye. Kijana huyu alizoea kuchunga mbuzi na kondoo malishoni. Ndugu zake waliposikia hivyo walimkataza na kumwambia kwamba mtu yule mbabe atamuua. Kijana huyu mdogo aliyeitwa Daudi aliwajibu na kusema "Mtu yule ni mnene Sana,  pande la mtu kiasi kwamba sitakosa pa kupiga." Alichukua mawe na kombeo Lake alilotumia kuchungia mbuzi na kwenda nalo kupambana na Goliathi.  Baada ya Goliathi kumuona kijana yule mdogo alicheka sana na kuona kwamba atamuua Daudi ndani ya sekunde kadhaa.   Daudi alichukua jiwe moja akaliweka kwenye kombeo lake na kisha kulizungusha na baadaye alilitupa kwa kasi sana. Jiwe lile lilitua katika paji la uso wa Goliath. Goliath alianguka chini na huo ukawa mwisho wake. " (Hadithi ya Biblia).

 Kumbe matatizo ni mtihani lazima tuufaulu. Tena kwa maksi zinazomelemeta na nzuri.
Kwenye mwaka 1929, lilitokea anguko kubwa la kiuchumi (Great Economic Depression) ambapo uchumi wa dunia nzima uliyumba. Baadaye mwaka 1930 na 1931, inasemekana watu wengi walikuwa matajiri zaidi ya ilivyowahi kuwa hapo mwanzo. Matatizo yaliwapa watu mitihani waliifanya na kufaulu na hatimaye wakapata utajiri mkubwa.

Katika nchi ya Misri ambayo imekumbwa na ukame muda mrefu. Imekuwa ikitumia mto Naili kumwagilia mazao yake kama matunda na mbogamboga. Leo hii nchi ya Misri ndiyo nchi inayolima matunda mengi barani Afrika kuliko nchi nyingine yeyote.

Kumbe tunapokumbwa na matatizo ndipo tunapopata fumbuzi za matatizo yetu. Matatizo ni mtihani,  lazima uufanye na kufaulu. Matatizo ni fursa ambazo hazionekani,  baadhi ya watu ndio wanaoziona na kuzitafutia fumbuzi na hatimaye kufanya maajabu makubwa. Kwenye kitabu changu cha Barabara ya Mafanikio nimeandika "Mlango wa fursa hauna alama za "vuta" au "sukuma" "

Mafanikio yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog).

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Angelo said...

Very nice brother