Monday 12 June 2017

Ushauri Wa Bure Kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano

Habari mpendwa msomaji wa makala haya ya Bideism Blog. Nikupongeze kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa makala hizi za blogu hii.

Leo hii ningependa kutoa ushauri wa bure kwa wadogo zangu waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu wa 2017. 

Kwanza kabisa niwapongeze kwa kufaulu vyema katika mitahini yenu ya kidato cha nne. Pili napenda kuwapongeza kwa kuchaguliwa kuingia rasmi kidato cha tano. Hongereni sana.
Niwakumbushe sasa kuwa mmekua na mnayonafasi kubwa ya kuachana na mambo ya kitoto.sasa hivi ninyi ni watu wazima si watoto tena.

Nimekuwa nikiulizwa Sana swali la kwamba ni kombi gani nzuri na yenye fursa kubwa za ajira. Na kitu hicho ndicho kinachonisukuma kuandika makala hii.

Ukweli ni kwamba kila kombi ni nzuri na ina fursa nyingi za ajira. Kuna mambo mengi ambayo wengi hawayafahamu nataka myafahamu.  Ukitaka kombi nzuri na yenye ajira nyingi na itakayokupa pesa nyingi baadae soma kitu unachokipenda.  Usisome kombi fulani kwa sababu tu rafiki yako kipenzi anaenda kusoma kombi hiyo. Usifuate mkumbo. Wengi wamepotea kwa kufuata mkumbo.

Usiende kusoma kombi Fulani kwa sababu tu umeshawishiwa na wazazi wako lakini wewe huipendi.  Soma kitu unachokipenda. Faida kubwa ya kusoma kitu unachokipenda ni kwamba unajiweka katika nafasi nzuri ya kufaulu katika mitihani ya kidato cha sita.

Jambo jingine kumbuka mnakokwenda mashuleni bidii yako ya kusoma ndiyo kufaulu kwako. Kuna msemo tumeuzoea unasema "Advance ni misuli yako." usisubiri kuletewa kila kitu umeze kama ilivyokuwa kwa kidato cha nne. Ukweli ni kwamba hatua uliyofikia walimu wa kukupa kila kitu ni wachache,  tena wengi wako shule za binafsi/private. Hivyo jiandae mapema vuta pumzi jiweke tayari kupambana na adui ujinga.

Nawatakieni masomo mema.

See You at the top.

Ndimi
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Washirikishe na wanafunzi wenzako makala hii iwasaidie.

Karibu Sana kuweka oda ya kitabu changu cha "Barabara ya mafanikio"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: