Friday 2 June 2017

Usihukumu Watu Hovyo Hovyo

Habari Za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism BLOG. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako siku ya leo. Tumshukuru Mungu kwa kutupa siku nzuri kama ya leo. Leo ni siku muhimu usikubalii ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana kwenye makala nzuri niliyokuandalia leo.

Jana kabla sijalala rafiki yangu anayeitwa Paul alinitumia video moja kupitia mtandao wa whatsapp ambayo ilinifunza kitu na kitu hicho hicho ningependa na wewe mpendwa msomaji ujifunze Pia.
Katika video niliyotumiwa ilikuwa kwenye mfumo wa hadithi. Video hii ilianza kumuonesha dokta mmoja akiingia hospitali kwa haraka sana huku akielekea chumba cha wagonjwa mahututi.
Alipofika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kuingia ndani alikutana na baba ambaye alimleta mwanaye aliyekuwa anaumwa vibaya sana na alihitaji oparesheni ya haraka sana.

Baada ya kufika na kukutana na bwana yule dokta aliomba msamaha kwa kuchelewa.
Baba yule alimwambia dokta "ungewahi hali isingekuwa hivi". Dokta alimjibu "kuwa mtulivu, mwanao atapona." Mzee yule kwa jazba akamjibu "angelikuwa mwanao ungesema hivyo?". Dokta akamjibu tena "Kwa Nguvu ya Mungu mwanao atapona" kisha akaingia kwenye chumba alipolazwa mgonjwa na kuanza kumfanyia upasuaji. Baada ya kufanikisha zoezi hilo daktari alitoka nje n.a. kisha kumpa mkono yule baba wa mgonjwa na kumwambia "hongera mwanao amepona." Huku akiondoka aliongezea maneno haya "maswali zaidi muulize nesi." Yule mzee alimuuliza nesi swali ili "mbona anajibu hovyo hovyo?" Nesi akamjibu "mwanae alifariki Jana kwenye ajali ya gari. Unavyomuona hapo Ametoka msibani kuja kuyanusuru maisha ya mwanao na sasa anarudi kuendelea na  msiba."

Hadithi hii  itufundishe kwamba, tusipende kuwahukumu watu bila ya kufatilia kuna nini nyuma. Na pia tusitamke maneno ya kuwaudhi wengine au kuwakwaza bila kujua ni nini kimesababisha hadi mtu unayemsema kakumbwa na kitu hicho. Mhamasishaji Les Brown wa Marekani aliwahi kusema "when you open your mouth you tell the world who you are."
 Akimaanisha "pale unapofungua kinywa chako, unaiambia dunia wewe ni nani."

See you at the top

Ni Mimi rafiki n.a. ndugu yako.
EDIUS BIDE KATAMUGORA
AUTHOR & MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com 

KARIBU SANA KUWEKA ODA YA KITABU CHA "BARABARA YA MAFANIKIO".

WASHIRIKISHE NA WENZAKO WAJIFUNZE KILE ULICHOJIFUNZA.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: