Saturday 8 July 2017

Historia Ikufundishe

Habari ya Leo mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako siku ya Leo.

Tumshukuru Mungu kwa kuiona siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako, usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia na ni matumaini yangu utajifunza kitu kipya kama ambavyo umekuwa ukijifunza kupitia makala ninazoziandika Mara kwa mara.

Mara nyingi maisha yetu yaliyopita yana mafunzo mengi ya kujifunza kwani maisha tuliyopitia yanasehemu kubwa ya elimu ambayo kama tungeitilia maanani tungejifunza kitu kikubwa ambacho tusingekubali kijirudie katika maisha yetu.

Kama uliwahi kujiingiza katika mahusiano mabovu na yasiyo sahihi, historia hii ikufundishe na usikubali mahusiano ya namna hiyo yajirudie.

Kama uliwahi kujihusisha na matendo maovu na tabia mbaya, ambazo zilikuwa zinakufanya usikubalike katika jamii inayokuzunguka, historia ikufundishe kwamba ulikokuwa siko, umejiweka sasa katika tabia na matendo mema.

Kama ulitumia pesa vibaya na hatimaye kujikuta katika umaskini uliopindukia, amka sasa usikubali maisha haya yajirudie.  Baada ya anguko kubwa la uchumi wa dunia mwaka 1929, inasemekana ndipo matajiri wengi walitokea hata kabla ya kutokea kwa tukio la anguko hilo. Kumbe wengi walijifunza kutokana na tulip hilo.

Kama ulikuwa husomi na ukashindwa kufaulu vizuri, historia hii ikufundishe kwamba unatakiwa sasa kuweka bidii na kusoma kwa nguvu zako zote na moyo mmoja ili kile kilichokwishwa tokea kisitokee tena au kisijirudie.

Kama ulifukuzwa kazi kisa makosa ya kiutendaji, nidhamu na makosa mengine yaliyotokana na uzembe wako. Jifunze na hakikisha makosa hayo hayajirudii tena kwenye maisha yako.

Siku moja Bill Gates ambaye ni tajiri namba moja duniani na mmiliki wa kampuni ya Microsoft alikwenda mgahawani pamoja na binti yake. Baada ya kupata kifungua kinywa Bill Gates alitoa dola $5 na kumpatia mhudumu alistuka kuona sura ya mshangao kutoka kwa mhudumu huyo. Ndipo alipoamua kumuuliza, "mbona unaonekana kushangaa, nini tatizo?" Mhudumu huyo alijibu "Nashangaa binti yako ametoa dola 500 na wewe tajiri namba moja duniani umetoa dola 5 tu!" Bill Gates alimjibu "Huyu ni binti wa tajiri namba moja duniani na Mimi ni mtoto wa mkata mbao (son of wood cutter)." Historia yako ni funzo tosha.

Historia yako hata kama ni mbaya vipi kuna kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuangalia ulikosea wapi ili makosa hayo yasijieudie. Ili ikupe motisha ya kufanya kwa bidii na juhudi ili baadae uwe mshindi.

Mafanikio yapo mikononi mwako

Ndimi
Edius Katamugora (Bide)
Author and motivational speaker
0764145376
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio sasa kinapatikana rasmi kwa mawasiliano yangu hapo juu. Mikoani tunatuma.

Imani yangu kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: