Saturday, 30 September 2017

Aina Za Elimu Mzazi Anazotakiwa Kumpatia Mwanae

"Kama malengo yako ni ya mwaka mmoja. Panda mpunga.
Kama malengo yako ni ya miaka kumi.
Panda miti.
Kama malengo yako ni ya miaka mia moja. Waelimishe watu." Alisema Confucius.
                    

Mojawapo ya vitu vinavyohitajika kwa mwanadamu ni Elimu. Kama Confucius alivyotamka hapo juu. Ukiwaelimisha watu ni sawa na kuwekeza kwenye kitu kikubwa.

Katika malezi na makuzi ya watoto kunahitajika aina nne za Elimu ambazo kila mtoto inabidi apatiwe ili kujiweka tayari kwenye maisha ya mafanikio.

Nitaelezea aina hizo nne za Elimu hapa chini:

1. Elimu ya Darasani (School Education):
Hii ndiyo Elimu ambayo watu wengi huifahamu. Kama mtu ameenda shule basi watu huamini kwamba ameelimika. Lakini kama mtu anakosa aina 3 zilizobaki bado kuna vitu vingi anavikosa.
Wazazi wengi wamejitahidi kuwapatia watoto wengi Elimu ya darasani. Wamejitahidi kuwasomesha watoto wao katika mashule mbalimbali.

2. Elimu ya Dini:
Watu wengi tunayoimani kuhusu Mungu tunaamini Mungu ndiye aliyetuumba na anayeendesha maisha yetu. Hivyo ni jukumu lako mzazi kumlea mwanao katika misingi bora ya kidini. Mfundishe mwanao jinsi ya kusali na mambo mengi yanayohusu dini. Mfundishe mwanao kumtanguliza Mungu mbele katika kila kitu.

3. Elimu ya Maisha:
Hapa ndipo wazazi wengi huchemka. Wanafikiri wakiwapeleka watoto wao shule tayari wamepata kila kitu. Ukweli ni kwamba shule haiwezi kumfundisha mwanao kila kitu. Unahitahi kumfundisha mwanao kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo. Unahitaji kumfundisha mwanao kuwa mtu mwenye busara na kumfundisha kutokujiunga na makundi mabovu ya vijana wanaofanya matendo maovu. Ukweli ni kwamba hakuna shule nzuri kuliko ya nyumbani. Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza kuliko walimu wa shuleni.

4. Elimu ya Pesa (financial Education);
Mwanao anahitaji kujua matumizi bora ya pesa. Mwanao anahitaji kujua namna nzuri ya kutumia pesa yoyote unayompatia. Usimpe mwanao pesa kila siku bila kujua anaifanyia nini hii itampa maisha magumu mbeleni hakija kukosa pesa flani. Mfundishe mwanao kuhusu kuandika bajeti na kuifata. Wazazi wengi hawajaweza kuwafundisha watoto wao elimu kuhusu fedha jambo ambalo linawapa watu wengi wakiwa wakubwa.

Kama wazazi wako hawakukufundisha elimu kuhusu fedha usiwalaumu. Muda bado upo unaweza kujifunza mengi ukiamua. Nakushauri utafute vitabu vya Robert Kiyosaki uvisome utajifunza mengi kuhusu Elimu ya fedha. Wazazi nao pia wanaweza kuvitumia vitabu hivyo vya Kiyosaki.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
 Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.


Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: