Karibu asilimia 50 ya mafanikio inatokana na mazingira. Kwa maana ya kawaida tunaweza kusema mazingira ni kitu chochote kinachotuzunguka.
Mazingira ndiyo sehemu anayoishi binadamu wa kila aina, vitu vyote vyenye uhai wa kila namna na visivyo hai. Tamaduni na tabia za watu hutokana na mazingira na sehemu walizokulia. Ndiyo maana kuna wakati utasikia watu wakisema "Huyu mtu ni wa wapi?" ili walinganishe tabia yako na mazingira unayotoka.
Mazingira Mara nyingi ndiko sehemu kubwa au matendo na shughuli nyingi za kibinadamu hufanyika. Kuna msemo wa kingereza unaosema "Ukienda Roma, Fanya kama Waroma wanavyofanya." Yaani "When in Rome, do as Romans do. " Waafrika wakaongeza na kusema "Ukienda sehemu wanapokula konokono lazima na wewe ule konokono."
Je unayasoma mazingira?
Hili ni swali ambalo inanipasa nikuulize mpendwa msomaji. Kama nilivyotangulia kusema mazingira yanabeba zaidi ya asilimia 50 ya mafanikio. Kwa lugha nyepesi naweza kusema, mafanikio ni mazingira.
Hili ni swali ambalo inanipasa nikuulize mpendwa msomaji. Kama nilivyotangulia kusema mazingira yanabeba zaidi ya asilimia 50 ya mafanikio. Kwa lugha nyepesi naweza kusema, mafanikio ni mazingira.
Kama haujui na hausomi mazingira unayoishi sio rahisi kufanikiwa. Kusoma mazingira ni aina au njia mojawapo ya kujitambua. Kama ukiona mazingira uliyopo ayafai kwako kufanya mambo au mafanikio unayoyataka inakubidi uondoke na utafute mazingira mengine yatakayoweza kukusaidia wewe kutimiza ndoto zako. Huwezi kwenda kwenye nchi kame na kutegemea kufanya kilimo cha umwagiliaji. Lazima utafute mahali penye mito na maziwa yatakayokusaidia kufanya kilimo hicho cha umwagiliaji.
Kwenye Biblia kuna hadithi ya mwana mpotevu ambaye baada ya kuona amekua alimuomba baba yake sehemu ya urithi na baba yake aliamua kumpatia mwanae sehemu yake ya urithi. Baada ya kupewa urithi, mwana mpotevu alikimbilia katika nchi ya ugenini. Huko alitapanya Mali zake ovyoovyo huku akifanya uasherati na matendo maovu. Baadaye alikumbwa na wimbi la umasikini akapatwa na njaa kubwa iliyoikumba nchi ile aliyokuwako. Akaomba kuifadhiwa na bwana mmoja mwenye shamba ambaye alimpeleka katika shamba lake la nguruwe. Ikafikia hatua akatamani kujishibisha na chakula cha nguruwe (maganda ya nguruwe).
Baadae alikaa na kuwaza "Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanakula na kusaza chakula chake baba. Nami nataabika hapa, nashiriki na nguruwe chakula kisichofaa. Yanipasa kurudi. Nitarudi na kusema baba yangu nisamehe nimekosa mbele yako na mbele yake Mungu."
Baada ya kuona hivyo mwana mpotevu aliamua kutoka katika nchi ile ya ugenini na kurudi kwa baba yake. Kabla ajafika mbali baba yake alimuona akamwenea na kumkimbilia na kumkumbatia huku akiwa na furaha. Yule mwanae akasema "Baba nimekosa mbele yako na mbele ya Mungu sisistahili kuitwa mwanao."
Yule baba yake akawaagiza watumwa wake "letene vazi lililo bora mumvike, mvike na Pete kidoleni pake." Wakampa na viatu.
Baba yake akaagiza wamchinje ndama yule aliyenona nao wakanchinja na kuanza kufurahi na kusherehekea huku baba yake akisema "Huyu ni mwanangu, alikuwa amekufa sasa amefufuka, alikuwa amepotea, ameonekana." Basi ikawa ni vifijo na sherehe nyumbani mwa bwana yule. (Luka 15:11-24)
Ukiangalia kwa haraka haraka kwenye hadithi hiyo hapo juu utatambua yakwamba mwana mpotevu aliyasoma mazingira na kutambua kwamba hayafahi ivyo akaamua kurudi kwao.
Wewe pia unahitaji kuyasoma mazingira. Jiulize je mahali nilipo na vitu ninavyovifanya vinanipeleka kwenye ndoto zangu. Donald Trump aliwahi kusema "Ili ufanikiwe yakupasa kujua kila kona na kila aina ya mti unaopatikana katika mazingira yake." Miaka mitano ijayo hakikisha unasema "Naishi maisha niliyoyachagua." Lakini hili litatokea endapo utayasoma mazingira. Yasome mazingira.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment