Wednesday, 13 September 2017

" Kama shule zingepewa jukumu la kuwafundisha watu kuongea na kutembea, wengi wangekuwa mabubu na viwete." Anasema Herbert Kohl mwandishi wa kitabu cha Reading, how to na pia mhitimu wa chuo cha Harvard.

Herbert ameyasema hayo akitaka kutuonesha kwamba shule haiwezi kukufundisha kila kitu inakupasa utafute maarifa nje ya shule. Kuongea na kutembea unajifunza nyumbani kabla ya kwenda shule.


                     
(Piga namba 0764145476 ili kupata kitabu hicho hapo juu)

Nakushukuru wewe kwa sababu umeamua kusoma makala hii kwa sababu nakufundisha mambo ambayo mwalimu wa darasani hawezi kukufundisha.

Wakati nikiwa kidato cha tatu katika kipindi cha Baiyolojia nilijifunza jaribio alilolifanya bwana mmoja aliyejulikana kama Pavlov. (Kama nilivyosema hapo juu, unaweza kujifunza shuleni lakini hauambiwi kinaendana kivipi na maisha ya kila siku).

Jaribio la Pavlov (Pavlov Experiment)

Bwana Pavlov alikuwa akifuga mbwa. Alizoea kuwapa chakula cha mchana kila ifikapo saa 7 kamili mchana. Lakini namna yake ya kuwapa chakula mbwa wake ilikuwa ya tofauti kidogo.
Kabla ya kuwapa chakula mbwa wake kwanza aligonga kengele ndipo alipowapelekea chakula mbwa wake.
Zoezi hilo alilifanya kwa muda mrefu sana. Siku moja akaamua kugonga kengele lakini hakubeba chakula. Kilichotokea ni kwamba akiwakuta mbwa wake wakitoka mate mdomono(salivation) kwa maana walijua wanaletewa chakula(walikua na hamu ya chakula).

Nimeandika uchunguzi/jaribio hilo la Bwana Pavlov Ili kukuonesha kwamba tabia yoyote inajengwa. Wahenga walisema "Mazoea hujenga tabia." Kumbe ukifanya kitu kwa muda mrefu utakifanya kiwe tabia yako.

Mfano ukisema nitaamka kila siku saa 11 alfajiri kama Mimi na kuanza kufuata ratiba hiyo kwa muda mrefu utajikuta hata huchoke vipi saa11 kabla ya saa12 lazima ushtuke toka usingizini tu.

Unataka kuanza kusoma vitabu, hakikisha kila siku unasoma walau kurasa tano. Ukifanya hivyo kwa muda mrefu hiyo itakuwa tabia yako.

Uchunguzi unaonesha kwamba tabia yoyote iwe mbaya au nzuri hujengwa ndani ya siku thelathini yaani mwezi mmoja. Kumbe unahitaji mwezi mmoja kujenga tabia mpya ambayo unatamani kuianza. Kumbuka kuanza nzuri tabia mpya sio rahisi wengi wanaweza kianzisha tabia mbovu zikadumu kwa muda mrefu kuliko tabia njema.

Mfano ilinichukua sana muda kuanza kuweza kuamka saa11 wakati watu wengi wanakuwa usingizini wakisema hakujakucha lakini Leo hii naona ni jambo la kawaida lakini nilipata maumivu makubwa. Muda mwingine nilitamani nipasue simu pale alamu ilipolia lakini nilipiga moyo konde na kusema lazima niamke. Leo hii imekuwa tabia yangu.

Je wewe ungependa kuanzisha tabia ipi nzuri?.
 
Unataka kuanza kuwahi kazini au darasani?

Unataka kuanza kufanya mazoezi kila siku?

Unataka kuandika makala za kuelimisha kila siku?.

Unataka kuanza kusoma vitabu kila siku?

Yote hayo yanawezekana kama ukichukua maamuzi ya kuanza kufanya kitu ulichopanga kuanza kukuifanya.

Kumbuka unahitaji mwezi mmoja bila kukwepesha siku hata moja. Ni maumivu lakini lazima uyakubaki kama unataka kufanikiwa kujenga tabia mpya. Ukiweza kuhimili siku 30 bila kukwepesha hata siku moja utakuwa umejijengea tabia yako mpya. Anza Leo kufanya kitu hicho usiseme nitaanza kesho, maana kesho huwa haiji. Tomorrow never comes.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
 Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: