*Maisha Yakibadilika Yakawa Magumu. Unabadilika Unakuwa Mgumu.*
Shalom mpendwa.
Leo hii katika Tanzania yetu hii kila mahali unapokwenda, kila mtu unayewasiliana naye anakwambia maisha ni magumu hamna pesa. Tena wameanzisha msemo na kusema "Vyuma vimekaza."
Ni kweli hali imekuwa chungu, pesa haipatikani lakini tunaitaji kubadilika. Ndiyo maana nasema "Maisha yakibadilika yakawa magumu unabadilika unakuwa mgumu."
Watanzania tunahitaji kubadili namna zetu za kufikiri. Maana hakuna umaskini mkubwa kama umaskini wa mawazo. Leo hii hata ukipoteza milioni mia kama uwezo wako wa kufikiri huko vizuri lazima pesa yako itarudi tu.
Utawezaje kuongeza uwezo wa kufikiri? Kwanza soma vitabu mbalimbali, fika kwenye semina mbalimbali na ukutane na watu wengine utengeneze connection.
Pili: *Ongeza utendaji kazi wako.* Kama ulikua ukifanya kazi kwa mazoea sasa hivyi unahitaji kubadilika na kuwa mtu mwingine tena. Unahitaji kuwa mtu mpya. Mfano wewe ni mfanyabiashara wa duka ulizoea kufungua duka saa 3 kila siku badili ratiba yako. Anza kufungua duka saa 12 kamili. Ongeza pia bidhaa, kama una kibanda cha mpesa fikiria ni mambo gani mengine unaweza kuyauza ili upanue biashara zako. Watu wengi hufanya kazi kwa masaa nane hadi kumi, siku nzima ina masaa 24, ukitoa sita ya kupumzika wanayoshauri wataalam wa afya unabaki na masaa 18. Kumbe unaweza kupata muda wa ziada na kufanya maajabu makubwa.
*Tatu punguza starehe:* wakati bado watu wanalalamika vyuma vimekaza bado kuna Lindi kubwa la watu wanaendekeza starehe. Pesa uliyokuwa ukitumia kwenye starehe anza kuitunza kidogo kidogo. Wahenga walisema "haba na haba hujaza kibaba." Kama kila wikiendi ulizoea kwenda kuangalia mpira huku ukitumia elfu tano, punguza sasa angalia mpira hata Mara moja kwa mwezi, utakuwa umasave 15000/= hicho ni kiwango cha chini.
*Nne punguza muda kwenye mitandao ya kijamii na TV.* Pamoja na watu kulalamika kwamba maisha ni magumu lakini kuna watu wengi wanapoteza nusu siku wakitazama na kufatilia maisha ya watu kwenye mitandao ya kijamii wala hamna wanalojifunza. Wengine TV wanaangalia siku nzima. Hivi umewahi kujiuliza rais angelikuwa anatizama TV siku nzima kama wewe hii nchi ingeenda?. Unahitaji kubadilika. Kama unatumia mitandao ya kijamii itumii kwa manufaa ya kujifunza. Achana na magroup yanayopiga stori kuanzia asubuhi hadi jioni. Hayo hayakujengi yanakubomoa.
Tano *Tafuta marafiki sahihi*. Watu wengi wameharibikiwa kutokana na aina ya marafiki wanaoambatana nao. Unahitaji kutafuta marafiki wanaowaza mbele, marafiki wenye fikra chanya. Tafuta marafiki wapambanaji, wanaojituma. Jumapili katika makala niliyoiandika nilielezea zaidi kuhusu marafiki hivyo sina jambo la kuelezea zaidi.
Sita *Tafuta plan B.*
Kama unaona pesa unayoifanyia kama mshahara haikutoshi, hauna budi kutafuta chanzo kingine cha kipato. Tafuta biashara unayoweza kukuingizia kipato nje ya ajira unayoifanya. Unahitaji kufikiria nje ya boksi, ndiyo maana nimeanza na kusema badili fikra zako.
Kama unaona pesa unayoifanyia kama mshahara haikutoshi, hauna budi kutafuta chanzo kingine cha kipato. Tafuta biashara unayoweza kukuingizia kipato nje ya ajira unayoifanya. Unahitaji kufikiria nje ya boksi, ndiyo maana nimeanza na kusema badili fikra zako.
Ukiyafuata hayo baadhi ya mambo niliyokwambia utaona mabadiliko makubwa. Maisha yamebadilika. Watanzania tunahitaji kubadilika pia.
*"Mafanikio yako mikononi mwako.*
Kumbuka: *Maisha yakibadilika yakawa magumu. Unabadilika unakuwa mgumu.*
Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji.
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com.
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji.
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment