Watu wengi waliofanikiwa ni watu wanaotimiza malengo yao. Ni watu walioandika malengo yao na kuyafanyia kazi.
Malengo ni mambo unayohitaji kuyatimiza au kuyatekeleza ndani ya muda unaojulikana. Kumbe kama kuna kitu unahitaji kukitimiza lakini haujakiwekea ukomo wake wa muda bado haujaweka malengo.
Mfano unaweza kusema mwaka huu nitaandika kitabu. Hapo unakuwa haujaweka vizuri malengo yako. Lakini mtu anayesema mwaka huu tarehe 18/9/2017 naanza kuandika kitabu na nitamaliza kazi hiyo tarehe 2/2/18. Mtu huyo ameweka malengo. Tena kama atakuwa ameyaandika ni vizuri zaidi. Kuna nguvu kubwa ya kuandika malengo yako kwani yanakupa motisha ya kufanya kitu Fulani kila siku endapo utayasoma kila siku.
Mambo 3 unayohitaji ili kutimiza malengo yako.
1. Nia
Wakati wanajeshi wa Tanzania wanaagwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere kwenda kwenye vita ya Kagera miaka ya 70 mwishoni alisema "Sababu ya kupiga tunayo, nguvu ya kumpiga tunayo na nia ya kumpiga tunayo." Kumbe nia ni kitu muhimu sana kwenye kuweka malengo. Nia ndiyo motisha yenyewe ya wewe kutimiza malengo yako.

Nia ni kiu iliyoko ndani yako. Ukihisi kiu lazima unywe maji ya kutosha. Watu wenye mafanikio walikuwa na kiu ya kutimiza malengo yao. Unahitaji pia kiu ya kutimiza malengo yako. Jiulize Leo nia ya kutimiza malengo yako ni ipi?
2. Nidhamu.
Hakuna mtu aliyefanikiwa ambaye hana nidhamu. Ukitaka kufanikiwa tanguliza nidhamu kwenye maisha yako. Iweke nidhamu mstari wa mbele. Kuhusu malengo unahitaji kuwa na nidhamu juu ya muda. Ukisema nitaamka kila siku kabla ya jua kuchomoza hakikisha unafanya hivyo kweli. Watu wengi waliofanikiwa na kutimiza malengo yao huamka saa 11 alfajiri hadi saa 12 kamili. Wengine wamediriki kuamka hadi saa kumi. Saa kumi na 11 kitaalam tunaiita ''Time of legends ". Je wewe unaamka sa ngapi kila siku. Je unatumiaje muda wako kila siku?. Au unapoteza muda.

Tafuta muda wa ziada ili kutimiza malengo yako. " Siku moja inayo masaa 24, ukitoa masaa 6 ya kupumzika utabaki na masaa 18. Watu wengi hufanya kazi masaa 8 au 10. Ukitoa kwenye 18 yanabaki 8. Swali ni je unayatumiaje hayo masaa 8?" Anasema Arnold Schwarzenegger, muigizaji wa filamu za ngumi na Gavana wa Marekani.
Nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama matumizi yako yanazidi pesa unazoingiza tambua kwamba wewe huna nidhamu ya pesa. Mfano unapokea mshahara laki 5 lakini kila mwezi unatumia shilingi laki 7. Tambua kwamba huna nidhamu ya hela na hauwezi kuweka malengo na kuyatimiza. Nidhamu ya pesa ni kitu muhimu.
Unahitaji ni nidhamu ya kawaida. Ninaposema nidhamu ya kawaida namaanisha nidhamu tuliyofundishwa na wazazi wetu na hata mashuleni. Waheshimu watu maana hakuna lengo utakalo litimiza bila kuwahusisha watu. Watu ni kitu muhimu sana kwenye mafanikio. Ndiyo maana Watu wengi siku hizi wanalia hawana connection. Kama huna heshima unafikiri nani atakupa hiyo connection?. Msemo wangu ni ule ule siku zote "Jiconnect na watu watakuconnect.''
3. Maamuzi.
Unahitaji kuwa mtu mwenye maamuzi ili uweze kutimiza malengo yako. Lazima hubadilike. Albert Einstein aliwahi kusema " Huwezi kufanya jambo lile lile na kutegemea matokeo tofauti." Lazima uwe mtu anayefanya maamuzi ya kubadilika na uanze kuyafuata mara moja. Kama ulizoea kwenda kupiga soga vijiweni lazima uache au unashinda kwenye magroup ya WhatsApp na Facebook unachati kutwa nzima lazima hayo mambo uyasahau.

Unahitaji kuwa mtu mpya ambaye kabla hukuwa. Watu wanapoanza kusema Fulani kabadilika jua kwamba kuna kitu umekifanya kama maamuzi ili kutimiza malengo yako. Watu wanapoanza kusema fulani kawa kichaa, ndiyo pointi yako ya mabadiliko.
Mhamasishaji Les Brown anasema "Kama usipoprogramu maisha yako, maisha yatakuprogram." Yaani "If you don't program your life. Life will program you."
Baada ya kutambua vitu vitatu unavyohitaji ili kutimiza malengo yako ni matumaini yangu kwamba utakuwa tayari kutimiza malengo yako ya hata hii wiki tunayoianza Leo.
Nikutakie wiki njema na yenye mafanikio. Kumbuka anza wiki yako na motisha. Usiuzunike kuona Leo ni jumatatu. Watu wengi wanaichukia jumatatu kama nini. Mfanyakazi anawaza kurudi kazini. Mwanafunzi anawaza kazi zile za darasani. Uchunguzi unaonesha asilimia kubwa ya watu huaga dunia kufuatia presha na mshtuko wa moyo kuanzia saa 9 usiku wa jumapili hadi saa 1 kuamkia Jumatatu. Hii ni kwa sababu tu wamebeba chuki na manun'guniko kuelekea siku kama ya Leo, Jumatatu. Ipende Jumatatu ujiepushe na mengi. Lakini pia kuipenda siku ya mwanzo wa wiki inakupa msukumo wa kuimaliza wiki yako vema.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
1 comments:
Kweli kaka
Post a Comment