Tuesday, 10 October 2017

Nitaanzisha Biashara Yangu 2017 IV

Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Bila Mtaji au Kwa Fedha Kidogo.

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima na umeamka salama Leo hii.

Katika makala zangu zilizopita nilielezea jinsi unavyoweza kupata wazo la biashara. Kama hukubahatika kusoma makala hizo bofya katika link inayofuata hapa chini:

 
Leo hii ningependelea kuongelea jinsi unavyoweza kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji au kuanza na pesa kidogo.

 
Unaweza kupata mtaji wa kuanzia biashara yako kwa kuangalia vitu vifuatavyo:
 
1. Kipaji.
Kipaji ni kitu unachoweza kukifanya kwa urahisi zaidi ya mtu mwingine yoyote. Kitaalamu wanasema kila mwanadamu huzaliwa akiwa na vipaji na ujuzi(skills) kuanzia 400-700. Lakini wapo watu wengi hawatambui vipaji vyao. Ndiyo maana kuna mtu aliwahi kusema "Everybody is gifted but some people never open their boxes." Akimaanisha "Kila mtu amezawadiwa lakini kuna baadhi ya watu hawajawahi kufungua maboksi ya zawadi zao."

"Kipaji ni kama kito cha thamani machoni pale yeye aliyenacho, kila kigeukapo hufanikiwa." (Methali 17:8).

Kuna watu wengi wanavipaji lakini wanadharau vipaji vyao. Lakini duniani humu watu wenye vipaji ndiyo wanapata pesa nyingi na umaarufu mkubwa. Tazama watu kama Mbwana Samatta, Michael Jordan, Diamond, May weather, Lionel Messi, Ronaldo CR, kutaja wachache wanavyofanya maajabu kwenye ulimwengu.

Kama bado hujatambua kipaji chako na namna ya kukibadili kikawa pesa nakushauri utafute kitabu cha "Kutoka Sifuri Hadi Kileleni" cha mwandishi Godius Rweyongeza (0755848391) unaweza kupata mengi kuhusu kipaji chako.

2. Elimu uliyonayo;
Jihm Rohn aliwahi kusema "Wewe ni maskini kwasababu watu hawajui lolote kuhusu wewe." Kuna watu wengi wana ujuzi wa darasani lakini wameuficha hawataki kuuonesha wanadai wamekosa kazi za kufanya ndiyo hao wanazunguka na barua kila ofisi kutafuta kazi.

Nilipohitimu kidato cha NNE mwaka 2013, nilikua nikifundisha tuition watoto wa shule za msingi na sekondari. Wa shule za msingi walikuwa 3, na sekondari 3, jumla watoto 6. Niliweza kutengeneza hadi laki moja na elfu ishirini (120000/=) kwa mwezi.

Je wewe elimu uliyonayo inakusaidia lolote? Angalia ni kwa jinsi gani elimu yako inaweza kukusaidia kukuingizia kipato katika mazingira uliyomo. Usifikirie kuanzia pakubwa anzia padogo lakini hakikisha unafanya kwa weledi mkubwa. Watu watakutafuta tu na utapata pesa. Kuwa mtu mwenye malengo na maono makubwa na yafanyie kazi kila siku.

3. Kutumia pesa ya wengine (Other people's money).
Mojawapo ya watu ninaojifunza kutoka kwao kuhusu maswala ya kifedha ni mwandishi Robert Kiyosaki. Yeye Mara nyingi husisitiza kutumia pesa ya watu wengi kuanzisha biashara na sio lazima huwe na pesa zako.

Unaweza kuchukua pesa kutoka kwa watu kama mkopo na kuanzisha biashara yako na kisha kurejesha kidogo kidogo.

Kumbuka unahitaji kuwa mtu mwaminifu hasa linapokuja swala la ukopaji pesa. Kama watu hawakuamini sio rahisi wewe kupata pesa ya mkopo toka kwa rafiki zako.

Tukutane kesho kwa mwendelezo wa makala hii.

Unaweza kuwashirikisha wenzako. Mafanikio ni kitu cha kushirikishana.

Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi, Mhamasishaji na Mjasiriamali.
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

 

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: