Wednesday, 4 October 2017

Nitaanzisha Biashara Yangu 2017

Siku za nyuma nilikuwa sipendi kabisa kusikia neno lolote kuhusu biashara. Sikupenda kabisa kusikia kuhusu ujasiriamali na mambo mengi yanayohusu biashara.

Baada ya kuanza kufunguka kiupeo niligundua yakwamba ili ufanikiwe kiuchumi lazima uwe mfanyabiashara au mjasiriamali. 

Jaribu kuchunguza watu wote walifanikiwa kiuchumi lazima kuna biashara wanayoifanya.

Kumbe hata wewe kama ulikua hupendi mambo yanayohusu biashara lazima ubadilike kama mimi uanze kuipenda biashara na ujifunze kuhusu ujasiriamali.
                                     


Kuna watu wengi walisema mwaka 2017 wataanzisha biashara flani lakini bado hadi Leo hii Oktoba hawajaanza kufanya kitu chochote. Wiki hii nzima nimekuandalia makala zinazohusu ujasiriamali. Ambazo zinaweza kukusaidia kuanzisha biashara yako.

Mjasiriamali ni nani?
Kuna maana nyingi za mjasiriamali lakini nimechagua maana moja ambayo husema Mjasiriamali ni mtu anayetatua matatizo katika jamii ili kutengeneza pesa.

Kumbe ili uitwe mjasiriamali lazima utatue matatizo ya watu katika jamii. Lazima uguse maisha ya watu katika jamii.

Mambo matatu unayohitaji unapotaka kuanza ujasiriamali.
Kuna mambo makubwa matatu ambayo kila mjasiriamali lazima awe nayo anapotaka kuanza kufanya ujasiriamali. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo;

1. Lazima uwe na huduma ambayo ni tatizo katika jamii;
Hapa mtu huingia katika jamii inayomzunguka na kuangalia matatizo yanayoizunguka jamii yake. Ndipo hutafuta suluhisho na kuanza kulifanya suluhisho kama biashara yake. Mfano: Kuna tatizo la utupaji takataka ovyo mtaani kwangu. Suluhisho: nitaanzisha kampuni ya kukusanya taka nyumba baada ya nyumba.

2. Je jamii inayopesa ya kulipia huduma yangu?
Jambo la pili la kujiuliza hapa ni swali Je jamii inayopesa ya kulipi huduma yangu? Kama ndiyo utakuwa umejiweka katika sehemu nzuri. Kwa kutumia mfano wa hapo juu unaweza kujibu hivi: Ndiyo jamii inayonizunguka ina watu wenye uwezo hivyo wanapesa ya kulipia huduma nitakayoitoa.

3. Je wapo tayari kulipia huduma yangu?
Hapa lazima utofautishe kati ya kuwa na pesa na utayari. Jamii yako inaweza kuwa na pesa lakini ikakataa kulipia huduma yako. Jiulize je huduma unayotaka kuitoa itakubalika kulipiwa.

Ukiweza kuyajibu maswali hayo hapo juu vizuri bila tatizo utakuwa umejiweka katika fursa nzuri ya kuanza ujasiriamali.

Tukutane kesho kwa mwendelezo wa makala hii.

Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
Email: ekatamugora@gmail.com

Unaweza kumshirikisha na rafiki yako anayependa kuwa mjasiriamali.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

mavazi ya nguo said...

I learn much through your posts. I think, I shall be someone different