JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA
Habari rafiki yangu ni matumaini yangu yakwamba wewe ni mzima wa afya na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee . One day can make you grow.
(Kupata kitabu cha Barabara Ya Mafanikio pichani. Tuwasiliane 0764145476/ 0625961842)
Baada ya Jana kuongelea Nitaanzisha Biashara Yangu 2017 Sehemu Ya Kwanza, Leo nitaingia na kuongelea sehemu ya pili.
Kama hukusoma makala ya Jana bofya hapa: Nitaanzisha Biashara Yangu 2017
Jinsi Ya Kupata Wazo La Biashara Linaloweza Kukutajirisha.
1. Anza na familia yenu.
Familia yako inaweza kuwa imeanza au inafanya Biashara flani tayari. Hivyo hamna haja ya wewe kutafuta wazo jipya la Biashara. Unaweza kuichukua Biashara ya familia yako na kuiboresha zaidi.
Familia yako inaweza kuwa imeanza au inafanya Biashara flani tayari. Hivyo hamna haja ya wewe kutafuta wazo jipya la Biashara. Unaweza kuichukua Biashara ya familia yako na kuiboresha zaidi.
Mfano kama kwenu mnafanya biashara ya nyumba za kupanga unaweza kuziboresha nyuma zile na zikazidi kuleta kipato zaidi.
Makampuni mengi yameendelea kudumu miaka nenda rudi kwa sababu kuna watu ndani ya familia zao waliendeleza biashara yao.
Ray Kroc alianzisha mgahawa unaoitwa Mc Donald's huko Marekani lakini hadi Leo unadumu ingawa alikwisha fariki.
Colonel Sanders alianzisha kampuni ya kuuza mgahawa inayoitwa KFC ambayo hadi Leo hii bado inadumu.
Hapa kwetu Tanzania kuna Mo Dewji tajiri namba moja Tanzania yeye pia alichukua biashara iliyokuwa ikifanywa na familia yake na kuanza kuiboresha. Leo hii ndiyo mwajiri namba 2 baada ya serikali akiwa na wafanyakazi takribani 25000.
Kuchukua wazo au biashara ya familia yako si kitu rahisi kwani watu wengi wameshindwa kuendeleza biashara za familia zao.
Hivyo tambua kuna kazi kubwa ya kuiboresha biashara hiyo. Siyo kazi ya kizembe.
2. Vitu unavyovipendelea kuvifanya (Hobbies).
Jack Canfield aliwahi kusema "Kama hakikufurahishi. Usikifanye." Yaani "If it ain't fun. Don't do it." Akitaka kusisitiza umuhimu wa kufanya vitu unavyovipenda. Ukifanya kitu unachokipenda utakuwa mtu mwenye furaha ndani yako muda wote. Hakuna kitu kibaya kama kufanya kazi usiyoipenda. Uchunguzi unaonesha kwamba zaidi ya asilimia 80% ya Wamarekani wanafanya kazi wasizozipenda. Sasa hapa kwetu nafikiri ni zaidi ya 85%.

Mimi napenda sana uandishi na uhamasishaji ndiyo maana sipati shida kukuandikia makala haya. Je wewe unapendelea nini?
Chukua kalamu na karatasi andika vitu vitano unavyovipendelea na toka humo andika ni biashara gani unaweza kizifanya.
Bill Gates na Paul Allen walipenda sana kompyuta hivyo iliwapelekea kutengeneza Software mbalimbali za kompyuta na hatimaye kufungua kampuni ya Microsoft.
Steve Jobs alipendelea kuchezea kompyuta pia akiwa, nyumbani kwao kwenye garage ndipo alipoanzisha kampuni ya Apple.
Colonel Sanders alipendelea kupika akaanzisha mgahawa maarufu wa KFC ambao Leo hii unapatikana kila kona ya dunia.
Ni kuache na swali je wewe unapendelea vitu gani unavyoweza kuvibadili kuwa biashara?
3. Kupitia kusafiri.
Wahenga walisema "Tembea uone." Ukisafiri utaona mengi ambayo kwenye sehemu nyingi hayafanyiki kama biashara. Unaweza kulichukua wazo la biashara uliloliona Musoma ukalipeleka Njombe likafanya kazi na likakuingizia pesa ya kutosha tu.

Jana kama biashara inaweza kufanyika mahali flani inaweza pia kupelekwa sehemu nyingine ya dunia na kufanya maajabu makubwa.
Jana kabla sijalala nilisoma post moja kwenye moja ya group la WhatsApp iliyosema "Ujasiriamali ni kuwahi. Ukiwahiwa umekwisha." Sikumbuki aliiandika nani atanisamehe kwa kutotaja jina lake hapa. Kumbe ukiwa mtu wa kwanza kuanza biashara ambayo kwenye mkoa, wilaya, mji, au mtaa wakohaikuwepo unaweza kupata mafanikio makubwa.
Ukisafiri jiwekee utaratibu wa kuona ni fursa gani mpya za biashara unaweza kizichukua na kuzipeleka mkoani au mtaani kwenu.
Jiwekee pia utaratibu wa kusafiri kila mwaka unapopata likizo. Hii itakusaidia kufunguka kifursa na kibiashara. Hata kama una biashara tayari unaweza kuona wenzako mkoa flani wanafanyaje biashara kama yako na kupata maarifa ya kuendeleza biashara yako.
Tukutane kesho kwa mwendelezo wa makala hii ambapo nitaendelea na mada niliyoianza Leo.
Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Usisite kuwashirikisha wenzako wajifunze pia.
Ndimi;
Edius Katamugora
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa Shilingi 6000 tu. Tuwasiliane 0764145476.
0 comments:
Post a Comment