Monday, 17 July 2017

Hizi Ndizo Kozi Zenye Ajira

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako siku ya Leo. Tumshukuru Mungu kwa uzima na kutupa siku njema kama hii. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika Makala ya Leo niliyokuandalia.

Mara nyingi hasa wikiendi hii nimekuwa nikipigiwa simu na kuombwa niwatajie watu kozi wanazoweza kusoma ambazo zinafursa kubwa ya ajira. Baada ya kuona hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi nikaona ni vyema niandike Makala hii ili kuwasaidia wengine wengi wenye tatizo kama hili. Kwa maana Zig Ziglar aliwahi kusema "Utapata unachokitaka kwa kuwasaidia wengine wapate kile wanachokipata." Ndiyo maana Leo nimejitoa kuandika makala hii.

Wakati kama huu ambapo watu wengi wanaomba nafasi za kwenda chuo, wengi wao huwa wanakuwa na mawazo mengi na hii ni kwa sababu tu wanashindwa kutambua ni kozi gani nzuri wasome na wasome chuo gani. Nakumbuka wakati nimemaliza kidato cha sita nlipata Shida hii pia.

Kiufupi Leo hii hakuna kozi yenye fursa za ajira kama unavyodhani wewe au unavyoambiwa. Siku hizi mambo yamebadilika sio kama zamani. 

Nakumbuka kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia yeye alipomaliza tu kidato cha sita alitaka kuajiriwa na shirika la posta ambapo aliombwa kupewa nafasi lakini yeye alikataa. Ikumbukwe kwamba miaka ile shirika la posta lilikuwa na pesa nyingi sana kwani barua ilikuwa njia kuu ya mawasiliano (Watu waliamini barua ni nusu ya kuonana).

 Wengine hata kabla ya kumaliza chuo, waliambiwa ukimaliza chuo utafanya kazi hapa au pale tena serikalini. Naomba nikuulize swali mpendwa msomaji hivi siku za hivi karibuni uliwahi kusikia mambo kama hayo?. Jibu ni HAPANA tena ya herufi kubwa.



(Hakikisha kitabu hiki umekisoma pale unapoanza chuo kitakusaidia sana ukiwa chuoni na hata baada ya kuhitimu, unaweza kukipata kwa bei ya shilingi 15000/= tu. Piga simu: 0764145476 utatumiwa popote ulipo)

Huko mitaani watu wengi wamekuwa wakiibuka na kuzisifia kozi Fulani kwamba zinafursa kubwa ya ajira lakini ukiangalia kwa jicho la tatu ni uongo mtupu. Kadri ya sensa ya mwaka 2012 kila mwaka wanahitimu wanachuo milioni mbili lakini wanaoajiriwa ni laki mbili tu. Nafikiri unapata picha ya kile ninachokisema.

Siku moja wakati namsikiliza Rais Kaguta Museveni wa Uganda alipokuwa nchini Tanzania huko Chato alisema, "Kazi za serikali ya Uganda zipo laki moja na elfu arobaini na nne, na huku jumla ya watu wa Uganda ni takribani milioni 40 serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mtu." Huu ni ukweli unaozikumba nchi nyingi duniani. Tatizo la ajira linaendelea kukua kila uchao.

Tusiende mbali zaidi, naomba nikukumbushe vizazi vitatu muhimu ambavyo viliwahi kuambiwa kozi Fulani Ina fursa kubwa za ajira lakini vikatelekezwa kama watoto wa mitaani. Vizazi hivyo ni vifuatavyo;

Kizazi cha sheria;

Miaka ya tisini hadi elfu mbili mwanzoni uliibuka usemi kwamba ukisomea mambo ya sheria utapata kazi moja kwa moja tena ya serikali. Watu wengi wakajiweka makini na kwenda kusomea mambo ya sheria, walipomaliza wakaajiriwa wachache wengine wakabaki wakizunguka na bahasha zao za kaki ofisi hadi ofisi.

Kizazi cha Teknolojia;

Mwaka 1998 simu ziliingia nchini Tanzania hivyo kukawa na uhaba wa watu wenye utaalamu na mambo yanayohusu teknolojia kama kufunga minara na kuendesha mitambo mbalimbali. Vile vile watu wakaambiwa ukisoma mambo ya IT na Electronics ajira ipo nje nje, kile kilichotokea kwenye kizazi cha sheria kikakikuta kizazi hiki pia.

Kizazi cha ualimu:

Kuanzia mwaka 2007 serikali ilionesha kupungukiwa na walimu hasa wale wa sayansi, hivyo watu wengi wakaanza kusomea ualimu kisa pengo la ajira lilionekana huko. Hii ilikuwa wazi pale tu mtu alipomaliza chuo akisomea shahada ya ualimu alipewa kazi moja kwa moja. Leo hii shilingi imetumbukia chooni. Hakuna tena ajira za ualimu kwa wingi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kidogo.

Wengi wataniuliza tunafanyeje sasa? Na Mimi siwezi kukuacha njiani lazima nikupe majibu sahihi na najua utanipenda.

Kwanza kabsa chagua kozi unayoipenda; asilimia kubwa ya watu wanafanya kazi ambazo hawana furaha nazo. Hii ni kwa sababu tu walisoma mambo ambayo hawakuyapenda. Ebu fikiria mtu toka jumatatu hadi ijumaa kila siku Masaa nane anafanya kazi ambayo haipendi na  haimpi furaha. Watu kama hawa wanakufa kwa msongo wa mawazo na presha. Usikubali yakukute chagua kusomea kitu unachokipenda.

Pili, usichague kozi kisa umeambiwa ina fursa za ajira; kumbuka upendo wa kozi unayoitaka utangulie, kila kazi Leo hii inazo fursa za ajira na kila kazi Leo hii haina fursa za ajira. Tatizo linakuja kwamba wengi wetu wanamawazo ya kuajiriwa, kama na wewe unawaza hivi ondoa kichwani mwako mawazo mgando (stinking thinking). Anza tokea Leo kufikiria kujiajiri. Kumbuka nimesema wahitimu watu milioni mbili na ajira zinatoka laki mbili kila mwaka.

Stephen Covey mwandishi wa kitabu cha 7 Habits of highly effective people anasema, "Ujuzi wa mtu hufa kila baada ya miaka miwili." Kumbe kama unasomea kitu na baada ya miaka miwili haujakifanyia kazi tayari unakuwa hauna thamani katika soko.

Bofya hapa kusoma: A LETTER TO ALL UNIVERSITY STUDENTS

Tatu, usisome kitu usichokipenda kisa umechaguliwa na wazazi; kumbuka kazi utaenda kufanya wewe na sio wazazi wako unahitaji sana kusomea kitu unachokipenda na baadae uje ukifanyie kazi.

 Imewahi kutokea huko Kenya ambapo baba mmoja alimlazimisha mwanae asomee udaktari wakati yeye alipenda uhasibu. Kijana akubisha alienda chuo na kusoma miaka mitano ya udaktari alipomaliza na kutunukiwa cheti tena cha first class (daraja la kwanza) alichukua kile cheti na kumpelekea baba yake na kumwambia hivi "Baba alitaka nisome udaktari, cheti chako hiki hapa, narudi Leo chuoni kusomea uhasibu." Kijana Huyo akarudi chuo kuanza masomo ya uhasibu.

 Baba yake machozi yalimtoka. Kumbe wazazi pia msiwalazimishe watoto wenu kusoma kozi wasizozipenda.

Ipo wazi kuwa wazazi wengi wamechangia kuua ndoto za watoto wao kwa kulawalazimisha kusoma mambo wasiyopenda kuyasoma.

Bofya hapa kusoma: MAMBO YA KUFANYA SERIKALI INAPOSEMA HAMNA AJIRA

Usisome kozi Fulani kwa mkumbo; watu wengine sijui wakoje, akiona rafiki yake kachagua hivi na yeye anachagua kama yeye, hii ni kufata mkumbo na kusema kweli utapotea. Chagua wewe mwenyewe ili hata ukifika chuo mambo yakawa magumu useme hii ni chaguzi yangu, na maji ukishayavulia nguo lazima uyaoge.

Kumbuka kozi unayoipenda itakupa wigo mpana wa kupata kazi unayoipenda na utaifanya kwa furaha maisha yako yote.

Sahau kuhusu kuajiriwa anza sasa kuwaza kuhusu kujiajiri toka hapo ulipo.

"Mafanikio yapo mikononi mwako."

Ndimi
Edius Katamugora
Author and Motivational Speaker
0764145476
0758594893
E-mail: ekatamugora@gmail.com

Kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO sasa kinapatikana. Tuwasiliane ili ujipatie nakala yako. Waliokisoma sasa wanachekelea, unasubiri nini wewe?. Tumia namba hizo hapo juu.

Kama utahitaji pia ushauri wa ziada kuhusu Makala hii tafadhari usisite kunishirikisha kwa mawasiliano yangu hapo juu. Nipo tayari kukusaidia muda wote.

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Washirikishe na wenzio Makala hii.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

5 comments:

Aj king said...

ma man

Aj king said...

Thank you fir the enlightenment

Edius Katamugora said...

Welcome anytime boss

Unknown said...

Hey Bruh!! I Appreciate your work. Goodluck!!!!

Unknown said...

Naomba ushauri nilitaka kuanza kusoma digital marketing pls naomba ushauri ni nzuri na inalipa...