Monday 31 October 2016

Utajuaje Kama Utachukua Muda Mrefu Kufanikiwa Kiuchumi.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na safari yako ya mafanikio katika maisha yako ya kila siku.

Katika maisha yako ya kila siku kuna mambo unayofanya ambayo upandisha uchumi wako au uurudisha katika hali duni.

Mambo yafatayo ukiyafanya yatakuchukua muda mrefu kufanikiwa kiuchumi:

1). Kama katika pesa unayoingiza hakuna kiasi chochote unachoweka akiba ili uje kuwekeza badae.

2) Kama huwezi kueleza namna gani pesa zako zinatumika, hauna bajeti na unanunua vitu bila mpangilio.

3) Kazi unayofanya inakupa kipato cha kukuwezesha kula,kulipa kodi,nauli na matibabu na hauwezi kubaki na ziada hata kidogo.

4) Huwa unakopa Mara kwa Mara kwa ajili ya matumizi ya msingi (basic needs) kama vile kununua chakula, mavazi, kulipa kodi n.k na si kukopa kwa ajili ya kuwekeza.

Kwa sababu yoyote kati ya hizo nne; Unao uamuzi binafsi wa kubadilisha mwelekeo. Usifumbie macho dalili hizo, zina uwezo wa kukufanya maskini wa kudumu. Usiseme haiwezekani, INAWEZEKANA kutoka katika maisha ya namna hii. La msingi ni kubadili mtazamo wa maisha yako kama unakumbwa na mambo niliyoyataja hapo juu.

Jifunze kuweka akiba katika kiasi chochote unachoingiza.

Kuwa na utaratibu wa kutengeneza bajeti na mtu wa kununua vitu vya msingi na vyenye manufaa (assets).

Jitahidi usiwe mtu wa kukopa ili ununue vitu muhimu (basic needs).

Ni Mimi rafiki yenu na ndugu yenu Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476
Whatsapp; 0625951842.
Instagram: @eddybide

Tukutane kesho kwa makala nzuri za kuelimisha na kukuinua katika maisha yako.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: