Wednesday 2 November 2016

Tabia 7 Zitakazokufanya Uwe Na Furaha Muda Wote.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na safari ya mafanikio katika maisha yako. Nakupongeza pia kwa kuwa mdau mkubwa wa makala zangu za kila siku.

"Safari ya maili elfu moja uanza kwa hatua moja" alisema Lao Tzu. Tumia hatua hizi ndogo kutafuta furaha zaidi katika safari yako ya maisha.

1.Amka mapema.
Kuamka mapema hutengeneza siku njema. Pata muda muafaka wa kuamka mapema. Mwisho wa siku utaona kama umeweza kufanya kitu Fulani katika Siku husika.

2.Kuwa Na Heshima.
Waenga wanasema "Jiheshimu ueshimiwe". Jiheshimu kwa kuvaa mavazi mazuri ya heshima. Ukijiheshimu utaweza kuhisi mwenye furaha muda wote.

4.Jifunze kusamehe.
Msamaha ni kitu muhimu kwa maisha ya mwanadamu. Ukitunza chuki unakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu zaidi ya unayemchukia.
Samehe kila siku kabla hujalala utakuwa mwenye furaha siku zote.

4.Kuwa mzuri kwa kila mtu.
Jifunze kumfanyia mambo mema kila mtu unayekutana naye katika maisha yako, awe ndugu, rafiki, hata mtu usiyemjua.
Kumbuka furaha sio kupendwa na kila mtu muda wote, ni kupendwa na watu wachache kwa mazuri unayofanya au unayowatendea.

5.Tunza afya yako.
Afya ni Mali. Tunza sana afya yako, unaweza kupata nafasi ya pili kwa mambo mengi, lakini huwezi kupata mwili wa pili. Kama mwili wako hauna furaha fikra zako haziwezi kuwa zenye furaha pia.

6.Kuwa Jasiri na sio msumbufu.
Watu wasumbufu muda mwingi huwa hawawasikilizi watu wengine na Mara nyingi ufuata tu maisha yao. Wanaojiamini, wanakubali kwamba kuna muda unafanikiwa na mwingine unashindwa na wanaendelea na maisha yao. Wasumbufu wakishindwa ujikuta wanahuzuni muda wote.

7.Tabasamu zaidi.
Tabasamu kila asubuhi, uenda kuna mtu anatamani tabasamu lako.
Sambaza wema kwa watu wanaikuzunguka, wema utakurudia.

Ni mimi rafiki na ndugu yako; Eddy Bide.
Tuwasiliane: whatsapp:0625951842
Intagram; @eddybide

Tukutane kesho kwenye makala nzuri kama hii.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

2 comments:

Innocent said...

Great man bide,ila komaa u upgrade kwenda kwenye complete website if possible itakua rahisi zaidi kufikia wadau kuliko hosting,Big up @ admin http://www.tarimeskani.cf

Edius Katamugora said...

Pmj mdau Wang.Asante kwa ushauri kaka, nitaufanyia kazi.