Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na kupambana kuyatafuta mafanikio.
Nikushukuru pia kwa kuwa mdau mkubwa wa makala za blog hii.
Je ni mara ngapi umekutana na watu wakitafuta ni biashara gani wafanye ili watoke kimaisha?. Leo hii bideism blog tunakuletea jinsi ya kupata wazo la biashara linaloweza kukutajirisha.
Ili kupata wazo zuri la biashara fuata njia zifuatazo;
1. Anza Na Familia Yenu.
Familia ni kikundi cha watu ambao wana undugu wa damu (blood related).
Endapo wazazi wako wanafanya biashara Fulani ambayo tayari imekwisha fanikiwa basi huna haja ya kuhangaika na kujaribu kwenda sehemu nyingine au kujaribu kwenda sehemu nyingine au kujaribu kufanya kitu kingine, unaweza ukaichukua ile biashara na kuamua wewe kuifanya I we bora zaidi.
Sisemi uwe na wazo la kuiga lakini nachosema ni kwamba watu wengi wanapokuwa na wazo la biashara kwenye vichwa vyao huwa wanakuwa na theories hizo wazo halijakuwa proven (halijahakikishwa bado) uwezekano wa kushindwa huko palepale).
Sasa unapokuwa na biashara ya mjomba wako au ndugu yako ambayo umeshaiona tayari imefanikiwa maana yake ni kwamba na wewe unaweza kuifanya ikawa na mafanikio mazuri. Kwa sababu utaifanya kwa moyo wote bila manunguniko kwa sababu ni kama yako na pia biashara kama hizi zinaondoa zana ya utumwa katika kazi yaani unafanya kitu chako sio cha mtu mwingine.
Kwa mfano je unamfahamu mtu tajiri kuliko wote hapa Tanzania ambaye ni Mohammed Dewji ambaye anaongoza kampuni ya Mohammed enterprises. Yeye baada ya kumaliza masomo yake nje ya nchi aliporudi hapa nyumbani aliamua kuchukua biashara ya baba yake alichofanya akaipandisha ile kampuni, akaijengea mazingira mazuri, akaipanua na kwa sasa ile kampuni ndio mwajiri mkubwa kuliko kampuni zote Tanzania. Ina waajiriwa zaidi ya 24000 na ndio kampuni kubwa kuliko yoyote ambayo sio ya kiserikali na kusababisha Dewji kuingia kwenye orodha ya mabilionea duniani.
Sasa yeye alichofanya ni kuchukua biashara ya babake na sio wazo jipya. Nirudie tena kusema hata mchanganuo wako wa biashara uwe mzuri kama hujaanza ile biashara yako hiyo tunaita nadharia kwa hiyo nenda na mawazo ambayo yamehakikishwa, hivyo basi tafuta matunda ambayo yako chini wewe kuyafikia halafu yafanyie kazi.
Mtu tajiri kuliko wote duniani anapenda kusema "Take an ordinary idea but give it an extra ordinary execution" jipatie wazo la kawaida kabisa lakini utendaji wa tofauti.
Kwa hiyo unaweza kuchukua wazo la kawaida tu na ukilifanyia kazi vizuri utakuwa na mafanikio.
Je familia yako inafanya biashara gani ambayo utaichukua na kuiendeleza?. Tujiulize ilo swali leo.
Tukutane kesho katika mwendelezo wa makala hizi.
Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane; 0764145476
Whatsapp; 0625951842
Instagram: @eddybide
"See you at the top".
0 comments:
Post a Comment