Saturday, 12 November 2016

Tusiishi Kwa Ndoto Ila Kwa Malengo

Kuna tofauti kati ya 'kuishi kwa ndoto na kuishi ndoto.' Ndugu, tukubaliane katika hili-maisha ni malengo na siyo ndoto.

Ndoto ni maono anayopata mtu usingizini na 'lengo' ni nia(dhamira ya kukamilisha jambo fulani).
Hivyo ndugu, tujitahidi zaidi kuyafanya maono (ndoto) yetu kuwa kweli kwa kuweka malengo katika maisha yetu. Hatuna budi kuzifanya njozi zetu kuwa malengo hivyo tuweze kuziishi.
utasikia mtu anasema "nimeota najenga jumba la kifahari angani!!! " Hivi ni kweli waweza kujenga nyumba angani!?   Hapa lengo lapaswa kuwa kujenga nyumba ambayo unaweza kuifanya kuwa ya kifahari. Hivyo ili kuishi ndoto yako hauna budi kupambana, kukazana kupata pesa ya kutosha kujenga nyumba ya kuishi kwanza ndio uweze kujenga jumba ulipendalo. Kwani hauwezi kupata kumi bila ya kuwa na moja.

Ndugu tujitahidi daima kuishi ndoto zetu kwa kujiwekea malengo yetu na kujitahidi kuyafikia. Jione una deni mwaka ukiisha na haujayafikia!/kuyakamilisha. Asanteni Sana.

Makala hii imeandikwa na rafiki yangu Evance Mujuni.
0657923679

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.