Friday, 11 November 2016

Tujifunze Nini Toka Kwa Trump

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog.
Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na safari ya kuyatafuta mafanikio.

Leo nitaweka mezani makala inayomuhusu raisi mpya wa 45 wa Marekani bwana Donald Trump.
Binafsi mimi nilimfahamu bwana Trump kama bilionea maarufu tu wa New York Marekani. Ni mtu ambaye aliwahi kuwa tajiri na  baadae kukumbwa na umaskini (broke) baadae tena aliibuka na kuwa bilionea. Trump hakusoma sana kama zilivyo CVs za maraisi waliopita wa Marekani kama Obama na George Bush.

Bwana Trump amekua mgombea uraisi wa Marekani akishindana kwa upinzani mkubwa toka kwa bi. Hilary Clinton mke wa raisi wa zamani wa Marekani. Bwana Trump kapitia katika wakati mgumu sana ikafikia hatua kila mmoja akajiaminisha Clinton ndo atakuwa raisi mpya.

Je tujifunze nini toka kwa Trump?
Kwanza kabisa Trump ni mfano wa kutuasa tuombe kazi yeyote hata kama hatukizi vigezo. Trump katika kampeni kakumbana na kashfa zilizo mfanya apoteze wapambe wake lakini hakukata tamaa alisonga mbele, leo hii sijui hao waliomkimbia watarudi wakiwa vichwa chini!. Unapoachwa na marafiki zako wakati wa shida usikate tamaa Mungu anataka kukuonesha marafiki wa kweli ni wapi.

Jambo la pili la kujifunza hapa ni umuhimu wa siku. Ni tarehe 9/11/16 iliyomfanya Trump ang'ae ajulikane zaidi ya ilivyokua kabla. Hii itamfanya aendelee vizuri katika biashara zake. Kuna mtu aliwahi kusema "one day can make you grow". Kumbe kila siku ina umuhimu katika maisha yetu tuitazame kwa jicho la pekee.

Jambo la tatu ni kwamba "you don't need a perfect person you need a right one". Kila siku muombe Mungu akupe right person sio perfect. Mke wa bwana Trump bi. Melanie ni mfano wa right person ni mwanadada mwanamitindo lakini kaibukia kuwa first lady wa Marekani. Wengine walimbeza kwamba amekopi hotuba ya Mke wa Obama lakini ndo ashakuwa first lady.

Asante kwa kuwa na Mimi mwanzo hadi mwisho mwa makala hii.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu Eddy Bide.
Tuwasiliane; 0764145476
Whatsapp:0625952842
Instagram: @eddybide

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: