Wednesday, 30 November 2016

Niambie Rafiki Yako Nikwambie Tabia Yako.

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog.
Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na unaendelea vizuri na maisha yako ya kila siku.
Leo ni siku nzuri kwako tena itakayokuwezesha kuzifikia ndoto zako. Usichoke.

"Niambie rafiki yako nikwambie tabia yako" ni msemo wa kiingereza. Marafiki ni watu wako wa karibu ambao unaongea nao kuhusu wewe ukiwa huru,unashirikishana nao siri zako nyingi, changamoto zako na mafanikio yako ya kila siku.

Marafiki ni watu tunaowapata mashuleni,vyuo,ofisini,kazini na kila mahali. Ni watu ambao kwa kiasi kikubwa tunawaamini,tunawasikiliza na wanatujua sisi nje na ndani. Kumbe rafiki zetu wanaweza kuwaambia watu kwa mapana jinsi sisi tulivyo. Rafiki Mara nyingi uwa wanatabia zinazoendana hii ni kwa sababu mtu anampata rafiki kwa kumvutia na Yale aliyonayo. Kumbe kitu ambacho wewe unacho ndicho kinakufanya uwe na marafiki. Kama unapenda Mpira utajikuta una marafiki wengi wanaopenda mpira,kama unapenda muziki lazima utakua na marafiki wanaopenda muziki. Ndio maana wakati tunasoma shule wale wenye akili walikua wakijitenga. Wahenga wanasema "kaa na waridi unukie". Matajiri ata siku moja awafanyi urafiki na maskini ni wao kwa wao. Wanajiita "corridors of power"kama anavyosema mwandishi wa kitabu cha Speared Bw. S N Ndungulu.

Kumbe tunapokuwa na marafiki tuangalie tabia zetu zinaendana,au tunapenda kufanya mambo yanayolandana. Kwani watu wengi wanatuhukumu kutokana na tabia za marafiki zetu wa karibu. Ukiwa na rafiki mlevi watu lazima wakutambue wew kama mlevi. Ukiwa na rafiki wa karibu mkorofi watu watakuona wewe ni mkorofi pia. Ukiwa na rafiki mwenye upeo na mstaarabu watu watakuona wewe pia kama mtu mwenye upeo na mstaarabu. Kumbe tunapotengeneza marafiki tuangalie ni rafiki wa namna gani.

Jambo jingine la kuzingatia pia ni kwamba tusiwe watu wa kufuata marafiki bali marafiki watufuate. Kama nilivyotangulia kusema unawavutia watu ili wawe marafiki zako. Ukiwa mtu wa kuwafata utakuwa mtumwa kwao na hawawezi kuona umuhimu wako kama ukuwavuta wewe.

Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
Eddy Bide.
Tuwasiliane;0764145476
Whatsapp;0625951842
Instagram;@eddybide

Usisahau kulike page yangu ya Facebook ==>
#bideismblog.

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: