Friday 2 December 2016

Mambo Muhimu Ya Kufanya Katika Mwezi Huu Wa Desemba.

Habari mpendwa msomaji wa makala za Bideism Blog.
Ni matumaini yangu kwamba umeiona siku Mpya salama kabisa. Tumshukuru Mungu kwani ndiye aliyewezesha siku hii.

Karibu katika makala ya Leo inayozungumzia "Mambo muhimu ya kufanya mwezi wa Desemba" Mwezi wa huu ndio mwezi wa mwisho kabisa wa mwaka. Ni mwezi ambao watu hutumia sana pesa,starehe nyingi na kujikuta wakiwa mifuko mitupu inapofika Januari  mwaka  mpya.

Yafatayo ni mambo ya kufanya katika mwezi huu.
1.Orodhesha Mafanikio yako.
Mafanikio ni chachu ya maendeleo. Ni hatua muhimu katika maisha ya mwanadamu. Wakati mwaka unaanza  kuna mikakati madhubuti uliweka ambayo ungeifanya katika mwaka huu wa 2016. Kumbe anza na kuorodhesha mafanikio katika malengo uliyokuwa umejiwekea.

2.Orodhesha  mambo ambayo hayakufanikiwa.
Sio jambo rahisi kwamba kila ulichopanga kukifanya katika mwaka huu kimefanikiwa. Kumbe kuna mambo hayakwenda sawa. Hivyo orodhesha mambo ambayo hayakwenda sawa na weka mikakati mipya ya kutimiza mambo hayo.

3.Weka Bajeti
Kama nilivyotangulia kusema mwezi huu ndio mwezi ambao watu wengi hutumia pesa ovyo na kujikuta wakiwa mifuko mitupu inapofika Januari. Weka bajeti mahususi itakayo kuwezesha  kuishi bila madeni. Kuna watu wengi wanasema "maisha bila madeni hayaendi" huu ni uongo ambao hupo miongoni mwetu na sababu kubwa ni kwamba. Uongo ukisemwa sana miongoni mwa watu hubadilika na kuwa ukweli. Tujifunze kuweka bajeti na kuifata bajeti tuliyojipangia.

4.Weka Malengo Mapya.
Katika mwezi huu yakupasa kuweka malengo mapya ambayo utayatimiza mwakani. Kuanza mapema ni ishara kubwa ya kufanikiwa. Ususubiri mwaka uanze na wewe ndio uweke malengo yako. Pia weka njia mbadala zitakazo kuwezesha kufikia malengo uliyojiwekea.

5.Ongeza Imani Yako.
Kama tunavyojua huu ni mwezi wa mwisho katika mwaka. Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotujalia. Yeye ndiye anayewezesha maisha yetu ya kila siku, ametupa afya,nguvu na akili. Kumbe kila wakati tukumbuke kusali kwani kupitia sala zetu Mungu anatusaidia.

6.Anza au endelea kusoma.
Jiwekee utaratibu kila siku wa kusoma vitabu,magazeti na makala mbalimbali zinazohusu mafanikio. Katika maandiko hayo tunakuta mbinu zinazoweza kutusaidia katika maisha yetu ya kila Siku. Kuna mtu aliwahi kusema ni katika vitabu tunakutana na watu maarufu duniani. Binafsi nimekutana na watu maarufu kama kina Trump,Edson Thomas,Steve Jobs,Billgates na wengine wengi. Ukisoma vitabu na makala mbalimbali wanakupa mbinu mbalimbali zilizowapelekea kufika hapo walipo. Bila kufanya hivyo hatutawahi kuwasikia wala kuwaona.

Endelea kusoma makala mbalimbali katika blog hii.

Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
Eddy Bide.
Tuwasiliane; 0764146476.
Whatsapp;0625951842.
Instagram:@eddybide

Usisahau kulike page ya Facebook #bideismblog

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: