Tuesday 20 December 2016



                             

 Habari rafiki yangu? Bila shaka unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. karibu katika siku nyingine ya makala za BIDEISM BLOG. Makala zitakazo kuhakikishia kusonga mbele kadiri unavyoweza ili kufikia ndoto zako.

Katika makala ya leo nitaongelea kitu kinachoitwa UOGA WA UPINZANI. Hii ni hali ya kushindwa kujiwekea mipango na kuiweka katika matendo, kwa sababu ya kufikri watu wengine watakufikiriaje, watafanyaje au watasemaje. Huyu ni adui mkubwa wa kupoteza nguvu za kutoendelea kufanya jambo Fulani, kwasababu linakuwa katika fikra za mtu husika, ambapo uwepo wake haujulikani.


Ebu tuangalie dalili za woga wa upinzani. Watu wengi uruhusu ndugu wa karibu, marafiki, na jamii kwa ujumla kuwashawishi  kwamba hawawezi kuishi maisha yao, kwasababu ya uoga wa upinzani.
Watu wengi wanakosea kwenye ndoa, kushindwa kuchuuza na kuishia maisha magumu na yasiyo na furaha, kwasababu wanawoga wa upinzani inayoweza kufata kama wakisahii   makosa yao. (mtu yeyoyote aliyepitia katika uoga huu anajua maumizi yaliyojitokeza, yameharibu mipango yake, kazi zake hata ule moyo wa kufanikiwa).
Mamilioni ya watu wanakataa kurudi shule, baada ya kuacha shule kwa sababu ya uoga wa upinzani. Kuna namba kubwa isiyyo hesabika ya watu wanoogopa kujikita katika MAJUKUMU Fulani kwa sababu ya uoga wa upinzani. Watu wanaogopa kujihusisha na biashara kwa sababu ya uoga wa upinzani. Katika hali kama hizi woga wa upinzani ni kubwa kuliko ile hamu ya kufanikiwa.

Watu wengi hukataa kujiwekea malengo makubwa au hata kupanga kazi watakazo kuja kuzifanya kwa sababu ya uoga wa upinzani kutoka kwa ‘’maraf      iki’’ ambao wanaweza kumwambia ‘’ Husiwe na malengo makubwa, watu watadhani umechanganyikiwa’’.  Messi ambaye ni mcheza  maaarufu duniani anasema ‘’ Niliuza chai mitaani ili nipate pesa za kunisaidia kufanya mazoezi uwanjani’’ alifanya hivo na hakujali watu wangesemaje kuhusu yeye. Leo hii nani asiyemfahamu Messi kwa uhodari wake wa kusakata kabumbu safi uwanjani. Ni kwa sababu alilenga pakubwa na hakusikiliza watu wanasemaje. Dunia imejaa wakatisha tama.

‘’ Ili ufanikiwe unahitaji kujifunza kupambana na woga wa kukataliwa( fear of rejection), kitu ambacho nilijiambia nafsini mwangu, ambacho wananifikilia sio biashara yangu. Kitu ambacho ni cha muhimu ni ninachofikiria kuhusu mimi ‘’ alisema Robert Kiyosaki mwandishi wa vitabu maarufu duniani.
Naye  bwana Tony Robbins alikuwa na haya ya kusema ‘’ siri ya mafanikio ni kujifunza kutumia maumivu badala ya maumivu kukutumia wewe, ukifanya hivyo unayaongoza maisha yako na usipofanya hivyo maisha yako yanakuongoza’’               . jitahidi uwaoneshe wale watu wanaokwambia jambo Fulani aliwezekana kwamba linawezekana ( Prove them wrong).
Nimegundua kwa mawazo mengi bado yanazaliwa, na yanaitaji pumzi ya maisha            ambayo kwayo yanahitaji kuwekwa katika mipango na kuwekwa katika utendaji wa haraka sana. Muda wa kulilea wazo ni pale linapozaliwa. Kila linapoishi linapata muda zaidi wa kukua. Woga wa upinzani umekuwa ni chanzo.kikubwa cha kuharibu mawazo ambayo hayafikii kwenye mipango na utendaji. Jenga ndani yako moyo wa kuendele kufanya kitu Fulani hata kama umekosa watu wa kukusadia (support). Baba wataifa Mwalimu J.K.Nyelele aliwahi kusema ‘’it can be done, play your part) akimaanisha inawezekana cheza nafasi yako.

Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
EDIUS BIDE KATAMUGORA.
Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp; 0625951842 ( tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu whatsapp)
email; ekatamugora@gmail.com

Endelea kusoma makala nzuri katika blog hii. ASANTE

''See you at the top''.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: