Thursday 22 December 2016

Nguvu ya "Mimi ni.."

Habari mpendwa msomaji wa Bideism blog.
Nimatumaini yangu kuwa umeamka salama katika siku hii nzuri yenye unono wa mafanikio katika maisha yako.

Imebaki wiki moja na siku kadhaa kuumaliza mwaka. Leo naomba nikufundishe kitu muhimu katika maisha yako. Kitu hicho ni nguvu ya ''Mimi ni".
Unapoamka asubuhi jinenee maneno mazuri juu yako, Mimi nimebarikiwa, Mimi ni jasiri, Mimi ni mzuri, Mimi ni mkarimu, Mimi ni mwenye uwezo na akili, Mimi ni mwenye vipaji. Ukianza kujinenea maneno mazuri kama ayo unavutia akili na fikra zako kama unavyojinenea. Wahenga wanasema maneno uumba.

Wewe ni mtu wa pekee sana katika uumbaji wa Mungu ndio maana katika mamilioni ya watu wote duniani umepewa alama za vidole tofauti yaani za peke yako. Ndio maana nasema wewe ni wa pekee. Kabla ya wewe kuzaliwa na wazazi wako, Mungu alikwisha kuumba wewe kichwani mwake na kukufanya kiumbe chake kizuri aswa.

Soma: maisha yetu ni kioo cha matendo yetu

Je ni kwanini tunajinenea maneno mabaya?. Unakuta mtu anasema; Mimi ni mbaya, Mimi ni muoga, Mimi sina akili, Mimi sina kipaji, mimi ni mzee. Unavyojisemea ndivyo unavyojivutia kuwa. Ukisema Mimi sina akili, hutawahi ata Siku moja kufanya vizuri darasani, ukisema Mimi ni muoga, hutowahi kuwa jasiri ata siku moja, ukisema Mimi sina kipaji hutawahi kuona vifurushi vya vipaji vilivyo ndani mwako. Uchunguzi uliofanyika unadai kila mtu anazaliwa na uwezo na vipaji 500 hadi 700, lakini ukisema sina kipaji utawahi kuona hata kimoja kati ya hivyo 500-700. Ukisema Mimi ni maskini wa kutupwa, kweli utakuwa maskini wa kutupwa. Ukisema Mimi ni MZEE,utaona ata mvi zinajileta kichwani pako na uso unakunjamana. Jifunze kujinenea maneno mazuri kila Mara asa unapoianza siku mpya. Maneno unayojinenea sasa ayayongelei asa wakati wa sasa yanaongelea wakati ujao. Ndio maana huwa napenda kusema ''usitazame pale tu chini ulipo tazama na juu unapoweza kuwa.''

Maneno ni kama Umeme ukiutumia vizuri utakusaidia kufanikisha mambo yako. Lakini ukiutumia vibaya utakulipukia. Hii ndio maana halisi ya maneno. Ukijinenea vitu vizuri mambo mazuri yatafata njia yako na ukijinenea mambo mabaya, mambo mabaya yatakujia tu.

Kuna watu wengine leo hii wanafikiri na kuyabeba vichwani Yale walioambiwa na wazazi, ndugu, marafiki,walimu na watu wengine, ya kwamba wao hawawezi, hawana adabu, hawana akili,ni waoga, ni wasumbufu. Na bado wakayabeba vichwani mambo hayo ambayo hadi leo yanawaathiri. Watu wakinena mabaya juu yako, maneno hayo yapite sikio moja na kutokea sikio lingine, usiyaweke kichwani pako. Jibariki leo na neno zuri mbele ya maneno haya ''Mimi ni..''
Maliza mwaka wako kwa kujinenea mazuri..

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
Whatsapp; 0625951842 ( tuma neno ''SUBSCRIBE'' niwe nakutumia makala Zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram:@eddybide

Endelea kusoma makala nzuri kutoka blog hii. Asante

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: