UJACHELEWA
Habari mpendwa msomaji wa Bideism blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama siku ya leo na unaendelea kupambana kuelekea mafanikio.
Je ni mara
ngapi umeshindwa kufanya kitu Fulani na
ukahisi umechelewa?. Umefeli mtihani na ukuweza kuendelea na masomo, umeanzisha
biashara au mradi Fulani haujafanikiwa, umeachwa na mpenzi wako au umetupwa na
ndugu jamaa na marafiki, umehachishwa kazi au umefukuzwa kazi. Je unahisi
umechelewa kimaisha?. Leo ninayofuraha kubwa kukwambia ujachelewa.
‘’ Anguka mara saba simama mara
nane’’ ni msemo wa
Kijapani. Kumbe tunapoangua tusibaki palepale chini hatuna budi kusimama na
kusonga mbele. Kama umefukuzwa kazi uenda ndio umefunguliwa milango yakupata
kazi nzuri zaidi yenye kukupa furaha na wakati mwingine yenye kipato zaidi.
Kama umeshindwa mtihani uenda huu ndio muda wako muafaka wa kufanya maajabu
mapya katika historia ya elimu yako. Kama
umeachwa na mpenzi wako uenda ndio muda muafaka wa kumpata mtu sahii wa
mahusiano yako. Kumbe bado ujachelewa. ‘’ Mabadiliko
makubwa yako mikononi mwako’’ alisema raisi wa zamani wa Marekani Bwana
John F. Kenedy. Ivo basi tusikate tamaa
kwani kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu. Jambo la msingi hapa ni kukaa chini
na kutafakari kwa makini mambo yaliyosababisha tuanguke na kuyarekebisha kwani
‘’ Mtu ambaye anafanya makosa na hafanyi
jitihada yoyote kuyarekebisha au kuyasahihisha
anakuwa anaendelea kufanya makosa ‘’ alisema Confucius. Usibaki tu
kuwaza kama umechelewa kwani msongo wa mawazo ni sanaa ya kutengeneza matatizo
ambayo hata kabala hayakuwepo. Unapocheleweshwa uenda ndipo unapolenga mahala
sahihi katika maisha yako kwani ili mshale ufikie lengo lazima uvutwe kurudi
nyuma. Kumbe kurudi nyuma si kuchelewa bali kulenga mahali sahii.
Bwana Brian
Acton mwanzilishi wa mtandao wa kijamii maarufu kama WHATSAPP mwaka 2009
alikataliwa kufanya kazi na kampuni ya YAHOO kama mwandisi wa kampuni hiyo.
Mwaka huo huo pia alikataliwa kuajiriwa na kampuni ya FACEBOOK. Alikwenda na
kubuni WHATSAPP mwaka huo huo wa 2009. Mwaka 2014 kampuni ya FACEBOOK iliununua
mtandao huo wa WHATSAPP kwa dola za Kimarekani zipatazo bilioni 2.8. leo hii ni bilionea. Huyu ni mfano wa
watu ambao labda tungesema wamechelewa lakini hakuchoka kupigana hatimaye
akafikia ziadi hata ya ndoto zake.
‘’
Dunia inapokusukuma kwenye magoti inakupa wakati muafaka wa kusali’’ alisema
Rum.
Tufahamu kwamba tunaitaji
kuweka juhudi kubwa ili kuyafikia malengo yetu. Tuondoe dhana vichwani mwetu
kwamba tumepotea njia, hata Roma haikujengwa kwa siku moja. ‘’ Mlango mmoja unapofungwa, mwingine
unafunguliwa , lakini wakati mwingi tunayaacha macho yetu yakiangalia kwa
majuto mlango uliofungwa kiasi cha kutoweza kuona mlango mpya uliofunguliwa kwa
ajili yetu ‘’ alisema Alexander Graham
Bell.
Mwandishi wa
kitabu cha RICH DAD, POOR DAD Bwana Robert Kiyosaki anasema kwambwa ‘’ Sijawahi
kuona mtoto mdogo anayejifunza kutembea na hasianguke, sijawahi kuona mtu
anayejifunza kuendesha baiskeli ambaye
hajawahi kuanguka, sijawahi kukutana na mtu ambaye aliwahi kupenda na hajawahi
kuumizwa na sijawahi ona mtu tajiri ambaye ajawahi poteza pesa’’. Raisi wa Marekani TRUMP anaongezea na kusema
‘’ ili ufanikiwe lazima uanguke mara
nyingi na katika kuanguka utajifunza mengi’’.
Hivyo basi
ndugu yangu na rafiki yangu usihisi umechelewa katika kile ulichozamilia ili
kufikia malengo na ndoto zako. Weka mbinu mpya, mikakati mipya itakayokuwezesha
kufikia malengo yako. Badili mtazamo wako, kuwa chanya, epuka watu
watakaokwambia hutoweza kwani wao sio wewe. Wakati wako ndio leo wakati wako
ndio sasa.
Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora.
Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp; 0625951842 (tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja whatsapp)
email; ekatamugora@gmail.com
Endelea kusoma makala nyingine nzuri kama hizi hapa. Asante
'' See you at the top''
0 comments:
Post a Comment