Tuesday 27 December 2016

Mafanikio Ni Huduma

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama. Leo ni siku nyingine tena yenye tunu bora ya kutuletea mafanikio.

Karibu sana katika makala ya leo niliyokuandalia.

Mpendwa msomaji ili ufanikiwe jitahidi kutoa Huduma. Watu watakulipa kutokana na Huduma unayoitoa.

Makampuni mengi yanaendelea sana leo kwa kutoa Huduma. Sio Huduma tu ni huduma bora. Ukiwahudumia watu vizuri watu watakulipa kwa ile Huduma unayofanya.

Soma: Tabia 7 zitakazokufanya uwe na furaha muda wote

Ebu jaribu kuchunguza, kuchukua mtu yeyote aliyefanikiwa tazama anachokifanya, mwisho wa siku utagundua anatoa Huduma.

Ukiwa mtoa huduma watu watakufata tu na watakuwa tayari kukulipa kwa Huduma unayotoa.

Unaweza kuta watu wawili wanafanya kitu kimoja, tuseme kwa mfano biashara moja lakini unakuta mmoja anaendelea zaidi ya mwenzake. Hii inatokana na Huduma bora anayoitoa zaidi ya mwenzake.

Soma: Namna ya kugundua kipaji chako

Ebu jaribu kuchunguza ukienda dukani unanunua bidhaa Fulani na kuacha bidhaa Fulani. Ni kwa sababu bidhaa ile ni bora yaani kampuni husika inatoa Huduma bora.

Jiulize leo ni maeneo gani utaweza kutoa Huduma katika jamii yako. Watu wana Shida, watu wana matatizo, ukitatua tatizo au Shida zao vizuri watu watakuwa tayari kukulipa kwa Huduma utakayowapa. Ukipata eneo husika la kutoa Huduma lifanyie kazi kila siku jiulize namna ya kuifanya bora. Nakuhaidi mafanikio makubwa.

Kwahiyo kumbe ni jambo jema kujifunza kutoa Huduma kila Mara inapohitajika.

Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora

Tuwasiliane;
0764145476
Whatsapp; 0625951842 ( tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: eddybide
Facebook page: bideismblog

Asante kwa kuwa msomaji wa makala za blog hii. Usisite kuwashirikisha wenzake unachosoma na kujifunza hapa.

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: